Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wanafunzi wajawazito wamganda Rais Magufuli
Habari za Siasa

Wanafunzi wajawazito wamganda Rais Magufuli

Spread the love

WANAFUNZI wa wanaopata ujauzito kutorudi shuleni wamezidi kumkera Rais John Magufuli kwani pamoja na kupiga marufuku, amekuwa akiendelea kuchimba ‘mkwara’ kila anapopata nafasi, anaandika Irene Emmanuel.

Rais Magufuli alishapiga marufuku wanafunzi wanaopata ujauzito kurudi shuleni na kuzuia asasi zisizo za kiserikali kuendelea kutetea hilo, lakini pamoja hayo bado amezidi kupinga kila anapopata nafasi ya kufanya hivyo.

Akiwa katika uzinduzi wa nyumba za wahudumu wa afya wilayani Chato, Rais Magufuli amerudia tena katazo hilo na kuzitaka taasisi zinazounga mkono hoja za kutetea wanafunzi wanaopata ujauzito kufanya kazi za maendeleo ya jamii.

Amesema kuwa hoja hiyo inakosesha heshima Taifa kwa kujenga picha ya ubakaji, kwamba si kila aliepata mimba amebakwa, wengine wanajitakia na kuruhusu hilo itapelekea wimbi la wajawazito mashuleni.

“Ati kila aliepata mimba amebakwa? Hata kwenye familia yangu wapo waliopata mimba, wala hawakubakwa. Wasije watu wakaharibu heshima na tamaduni za kitanzania zilizojengeka muda mrefu” Alihoji Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameziomba taasisi zingine ziige mfano wa taasisi ya Mkapa Foundation kufanya mambo ya maendeleo na wasiishie kupiga kelele majukwaani, taasisi ya Mkapa imejenga nyumba 450 huku zikiwa zimebaki nyumba thelathini.

Ameendelea kwa kuitaka serikali kusaidia kifedha taasisi kama ya Mkapa Foundation zinazojali maendeleo na kuzinyima fedha taasisi zile zinazounga mkono watoto kupata mimba na kuzaa wakiwa shuleni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

Habari za Siasa

Babu Owino: Vijana msibaki nyuma

Spread the loveMbunge wa Embakasi Mashariki nchini Kenya, Paul Ongili Owino maarafu...

error: Content is protected !!