Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanafunzi wa kiume Z’bar hatarini
Habari Mchanganyiko

Wanafunzi wa kiume Z’bar hatarini

Kisiwa cha Zanzibar
Spread the love

IMEELEZWA kuwa jumla ya watoto wa kiume wapatao 40 wanaosoma kati ya darasa la kwanza na la tatu kutoka visiwani Zanzibar wamefanyiwa ukatili wa kuingili kinyume na maumbile, anaandika Dany Tibason.

Hayo yameelezwa na Meneja wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi, haki za watoto na vijana, Dk. Ellen Otaru wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la madhimisho ya Vijana Duniani lililofanyika kitaifa mjini Dodoma.

Dk. Otaru amesema kutokana na vitendo vya ukatikili wanavyofanyiwa watoto hao wa kiume kunaweza kuwasababishia madhara makubwa ya kiafya endapo watakosa msaada wa kimatibabu kwa kuwarejesha katika hali yao ya kawaida.

Amesema sababu kubwa ya watoto kufanyiwa vitendo vya kinyama kwa kuingiliwa kinyume na maumbile ni kutokana na kutotolewa kwa elimu ya afya ya uzazi mashuleni.

Dk. Otaru mesema elimu ya afya ya uzazi inatakiwa ianze kutolewa mashuleni kuanzia shule ya awali tofauti na sasa elimu hiyo inaanza kutolewa kuanzia miaka 10 badala ya sita.

Amesema kama elimu ingetolewa mapema ni wazi kuwa watoto wa kiume wangejua mapema kujikinga na watu wenye nia mbaya ya kutaka kuwalawiti huku watoto wa kike wakiwa na maarifa ya kujiepusha na upatikanaji wa ndoa na mimba za utotoni.

Hata hivyo ameitaja mkoa wa Shinyanga unaongoza kwa tatizo la mimba za utotoni kwa asilimia 53 ukifuatiwa na mkoa wa Tabora na huku akieleza kuwa vitendo hivyo havitokani na umasikini tu bali hata ukosefu wa elimu kwa jamii.

Pia alitoa wito kwa wazazi/walezi kuzungumza na watoto ili kuweza kupata elimu ya afya ya uzazi ambayo itawasaidia na kujua madhara atakayoyapata akitenda jambo hilo badala ya kuwaogopa watoto.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!