Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko “Wanafunzi vyuo vikuu wanashiriki mapenzi ya wenyewe kwa wenyewe”
Habari Mchanganyiko

“Wanafunzi vyuo vikuu wanashiriki mapenzi ya wenyewe kwa wenyewe”

Spread the love

SHIRIKA la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto (Kivulini) mkoani Mwanza, limebaini vijana wengi wa vyuo vikuu hususan wa mwaka wa kwanza, wamekuwa wakitumia mikopo ya elimu ya juu kujiingiza katika mapenzi ya wenyewe kwa wenyewe. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kivulini, Yassin Ally mbele ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella wakati wa uzinduzi  siku ya Ukimwi yaliyokwenda sambamba na maadhimisho ya  siku 16 za kupinga ukatili wa jinsia yanayofanyika kitaifa mkoani Mwanza.

Alisema maambukizi kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 -24  ni asilimia 40 kiwango ambacho ni kikubwa ambapo alifafanua kuwa  hivi sasa kundi hilo haliogopi tena Ukimwi badala yake linaogopa mimba huku wakiwa watumiaji wakubwa wa kuweka vitanzi na kinga zingine.

“Leo hii vijana hawaogopi Ukimwi bali wanaogopa mimba, asilimia karibu 80 ya wanafunzi wa jinsia ya kike wa vyuo vikuu wamejiwekea vitanzi na kinga zingine ili wasipate mimba, ndio maana wanavyuo hasa wa mwaka wa kwanza jinsia ya kiume wakipata mikopo wanakimbilia kuvalishana pete na wasichana wakiahudiana kama wameoana lakini hakuna ndoa mbeleni.

“Hali hii inatokana na jinsia ya kike kuweweseka kutafuta wanaume wa kuwaoa, sote tunajua suala la wanawake kuoana limekuwa gumu sana na si kwa wanavyuo pekee hata wanawake wakubwa mitaani wanatafuta mapenzi na wanafunzi.

“Kama mnavyoona hapa tumeamua kuwaalika wanafunzi wa vyuo vyote mkoa wa Mwanza ili ndani ya siku 16 hizi tutakuwa na midahalo kadhaa ili kujadiliana namna ya kupambana na ukatili na kuepuka ngono inayosababisha maradhi, jambo ambalo tunajivunia kama Kivulini tumefanikiwa kutokemeza ukatili wa wanawake katika Wilaya ya Magu na Misungwi,” amesema.

Hata hivyo katika uzinduzi huo viongozi mbalimbali kutoka mashirika ya kimataifa na kitaifa yamehudhuria ambapo watashiriki kutoa elimu katika midahalo kadhaa itakayohusisha wanavyuo mbalimbali huku kilele chake kinatarajiwa kufanyika Novemba Mosi, mwaka huu na mgeni rasmi ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika Mkoa wa Mwanza yameendelea kuongezeka kutoka asilimia 4.2 mwaka 2012 hadi asilimia 7 kwa mwaka 2016/17 huku kundi kubwa la waathirika ni vijana wenye umri kati ya miaka 15-24.

Mongella aliyemwakilisha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema ya Serikali imekuwa ikiweka mikakati kadhaa ya kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi lakini kundi la vijana mkoani humo limeendelea kuwa waathirika wakubwa kutokana takwimu kupanda kutoka asilimia 4.2 mwaka 2012 hadi asilimia 7 mwaka 2016/17.

“Takwimu hizi katika mkoa wa Mwanza zinakuwa kutokana na kuwapo na na visiwa ambavyo wakazi wa huko ni wavuvi na shughuli wanayofanya inachangia hali hii, mpaka sasa kama Serikali tunaendelea kuona namna ya kufanya kwa kushirikiana na wadau ili vijana wasiendelee kuangamia, tunataka wawe vinara wa katika mapambano ya Ukimwi.

“Tunaomba mashirika na wadau wengine kuungana ili kushusha kiwango cha maambukizi kwa vijana wetu maana tunaona Mkoa wetu unazindi ahata asilimia ya maambukizi ya kitaifa ambayo tunaelezwa ni asilimia tano, sote tunajua leo tumefanya matukio mawili kwa pamoja likiwamo la Ukimwi na siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, naombeni Mfuko wa Udhibiti wa Ukimwi Tanzania uweze kuniachia maboksi 30 ambayo nitahamasisha wakazi wa Mwanza kwa ajili ya kuchangia fedha ambazo zitasaidia katika mapambano,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

error: Content is protected !!