January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanafunzi, shule 10 bora kitaifa Upimaji Darasa la Nne (SFNA) – 2021, hizi hapa…

Spread the love

 

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne ambapo takwimu zinaonesha kuwa mwanafunzi bora kitaifa ametokea katika Shule ya Msingi Libermann iliyopo mkoani Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Aidha, shule 10 bora kitaifa katika matokeo hayo, takwimu zimeonesha kuwa mkoa wa Mara umeshika namba moja na namba mbili.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo tarehe 15, 2022 na Katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk. Charles Msonde pia yameonesha mkoa wa Shinyanga umechomoza na wanafunzi wanne katika kundi la wanafunzi 10 bora kitaifa na kufuatiwa na Lindi wenye wanafunzi watatu, Arusha wawili kisha Dar es Dar es Salaam ni mmoja pekee aliyeshika nafasi ya kwanza.

Aidha, katika kundi la Shule 10 bora kitaifa, mkoa wa Mara umechomoza na Shulen ya Twibhoki iliyoshika nafasi ya kwanza na kufuatiwa na Graiyaki iliyoshika nafasi ya pili.

 

error: Content is protected !!