June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanafunzi laki saba kuhitimu darasa la saba

Spread the love

JUMLA ya wanafunzi 775,729 wa darasa la saba wanatarajia kufanya mtihani wao wa mwisho wa kuhitimu elimu ya msingi, utakaofanyika kuanzia Septemba 9 na kumalizika Septemba 10, 2015. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania, Dk. Charles Msonde amesema wanafunzi hao wanatoka katika shule 16,096 nchini kote.

Dk. Msonde amesema kati ya wanafunzi hao wavulana ni 361,502, ambayo sawa na asilimia 46.6 na wasichana sawa na asilimia 53.4, huku wanafunzi wasiona ni 76, wavulana wakiwa 49 na wasichana 27, ambao watatumia maandishi ya nukta nundu katika kufanya mitihani hiyo.

Amesema maandalizi yamekamilika na baraza lipo makini kwa kuzuia udanganyifu wa aina wowote huo katika mtihani huo na watachukua hatua kali kwa yeyote atayefanya udanganyifu pamoja na kufutiwa matokeo.

“Kila kitu kimekamilika kuelekea kwa mtihani huo, kinachosubiriwa ni muda ufike na wanafunzi hao wafanye mtihani huo. Bazara tutachukua hatua kali kwa atakayejaribu kufanya udanganyifu,” amesema Dk. Msonde.

Dk. Msonde amesema masomo yatakayotahiniwa ni matano, ambayo ni kiswahili, hisabati, maarifa ya jamii, sayansi na english language.

Amesema wanafunzi watakaofanya mitihani hiyo kwa lugha ya kiswahili ni wanafunzi 748,514 na 27,215 kwa lugha ya kiengereza lugha ambazo walizokuwa wakizitumia katika kujifunza.

Aidha amesema kuwa kamati za mitihani za kila mkoa zinatakiwa kuhakikisha utaratibu unafuatwa hususani kipindi hiki cha kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu.

error: Content is protected !!