April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wanafunzi kumi  bora darasa la 7

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde

Spread the love

BARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta), limetangaza watahiniwa kumi bora Kitaifa katika matokeo ya kumaliza elimu ya msingi uliofanyika tarehe 7 na 8 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Matokeo hayo, yametengazwa leo Jumamosi tarehe 21 Novemba 2020 na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde ambayo yanaonyesha watahiniwa 833,672 kati ya 1,008,307 waliotunukiwa matokeo wamefaulu.

Dk. Msonde amesema, watahiniwa hao wamepata alama 100 au zaidi kati ya 250.

“Idadi hii ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 82.68. Kati ya hao wasichana ni 430,755 ambao ni sawa na asilimia 82.24 na wavulana ni 402,917 sawa na asilimia 83.15,” amesema Dk. Msonde.

Amesema, mwaka 2019, watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia 81.50 “hivyo, kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 1.18.

Katika matokeo hayo, yanaonyesha, kati ya wanafunzi kumi bora kitaifa, wametoka mikoa mitatu kwa mgawanyo wa wanne wametoka mikoa ya Mara na Shinyanga na wawili jijini Mbeya.

Haya hapa majina ya wanafunzi, shule na mikoa. Pia, kuna mgawanyo wa wavulana kumi bora na wasichana.

error: Content is protected !!