March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wanafunzi 917,072  darasa la Saba kuhenyeka kesho

Wanafunzi wakijisomea

Spread the love

WATAHINIWA  917,072 kutoka shule 16, 583 wanatarajia kuanza mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi (darasa la saba) kwa mwaka 2017 kuanzia kesho, anaandika Faki Sosi.

Baraza la Mitihani la Taifa  (Necta), limetangaza hayio leo huku likionyesha wale watakaofanya udanganyifu wa aina yoyote kwa kuwa watakumbana na mkono wa sheria.

Mitihani hiyo itafanyika kwasiku mbili yaani kesho na keshokutwa kwa nchi nzima.

Katibu mtendaji wa NECTA, Dk Charles Msonde aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Dk. Msonde amesema watawachukulia hatua wale wote watakaofanya udanganyifu ikiwamo kuwafutia matokeo yao.

error: Content is protected !!