July 31, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wanafunzi 500, walimu wao wajisaidia migombani

Spread the love

ZAIDI ya wanafunzi 500 na walimu watatu wa Shule ya Msingi Luholole kwenye Kata ya Kibuko, Wilaya ya Morogoro Vijijini, wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na kukosa vyoo, anaandika Christina Raphael.

Utafiti uliofanywa na Mtandao wa Habari za Kijinsia (TGNP) kwa kushirikiana na wanahabari mjini hapa umebaini kuwa, jumla ya wanafunzi 535 pamoja na walimu wao watatu wanajisaidia kwenye migomba iliyopo pembeni mwa shule hiyo kutokana na kukosa vyoo shuleni hapo.

Obed Simkanzya, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo amekiri kuwa walimu na wanafunzi wake wanajisaidia kwenye migomba kutokana na kukosa vyoo.

Anasema, tangu shule hiyo ianzishwe mwaka 1973, imekuwa inakabiliwa na ukosefu wa vyoo, na hivyo wanafunzi, walimu na wafanyakazi wengine hujisaidia kwenye migomba hiyo.

Kutokana na hali hiyo wanafunzi wamekuwa wakiugua mara kwa mara.

Vile vile, wanakabiliwa na ukosefu wa maji, madawati na samani za ofisi; wana miundombinu duni na upungufu mkubwa wa walimu.

“Uwezekano wa watoto kupata magonjwa ya milipuko ni mkubwa sababu wengine hucheza kwa kufukua michanga jirani na vilipo vinyesi vilivyokauka,” amesema.

Mtandao huu ulishuhudia watoto wasiovaa viatu wakicheza michezo mbalimbali na kuchimba udongo jirani na maeneo hayo bila tahadhari.

Shiwa Chalo, Mwenyekiti wa Kamati ya shule hiyo, anasema, matatizo ya vyoo yanatokana na wananchi kukatishwa tamaa na serikali kwa kushindwa kusaidia nguvu za wananchi kwenye shule hiyo.

error: Content is protected !!