September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanafunzi 422,388 wafaulu mtihani Kidato cha nne (2021), ufaulu waongezeka

Wanafunzi wa kitado cha sita wakifanya mtihani

Spread the love

 

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2021 ambayo yameonesha jumla ya watahiniwa wa shule 422,388 sawa na asilimia 87.30 kati ya ya watahiniwa 483,820 wenye matokeo ya kidato cha nne wamefaulu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo tarehe 15, 2022 na Katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk. Charles Msonde yameonesha wasichana waliofaulu ni 218,174 sawa na asilimia 85.77 na wavulana ni 204,214 sawa na asilimia 89.00

Amesema mwaka 2020 watahiniwa 373,958 sawa na asilimia 85.84 ya watahiniwa wa shule walifaulu mtihani huo.

“Hivyo, ufaulu wa watahiniwa wa shule umeongezeka kwa asilimia 1.46 ikilinganishwa na mwaka 2020.

Kuhusu ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya I – III ni 173,422 sawa na asilimia 35.84 wakiwemo wasichana 75,056 (29.51%) na wavulana 98,366 (42.87%).

Amesema mwaka 2020 watahiniwa waliopata ufaulu wa madaraja I – III walikuwa 152,909 sawa na asilimia 35.10. Hivyo, ubora wa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 0.74.

error: Content is protected !!