May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanafunzi 214 wafutiwa matokeo, 555 wazuiliwa

Dk. Charles Msonde, Katibu Mtendani wa NECTA

Spread the love

 

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza kufuta matokeo yote ya watahiniwa 214 waliofanya udanganyifu katika upimaji kitaifa wa darasa la nne, kidato cha pili, mtihani wa kidato cha nne na mtihani wa maarifa (QT). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Katika matokeo ya yaliyotangazwa leo tarehe 15, 2022 na Katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk. Charles Msonde yameonesha kuwa kati ya watahiniwa waliobainika kufanya udanganyifu, watahiniwa 83 ni wa Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne (SFNA).

“Watahiniwa 27 ni wa Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA), 102 ni wa Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Watahiniwa 02 ni wa Mtihani wa Maarifa(QT).

Amesema hatua hiyo imechukuliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 (2) (i) na (j) cha sheria ya Baraza la Mitihani sura ya 107 kikisomwa pamoja na Kifungu cha 30(2) (b) 2016 cha Kanuni za Mitihani.

Akizungumzia kuhusu matokeo ya watahiniwa 555 yaliyozuiliwa, Dk. Msonde amesema watahiniwa hao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya upimaji/mtihani kwa masomo yote au idadi kubwa ya masomo.

“Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kufanya upimaji/mtihani kwa masomo ambayo hawakuyafanya kwa sababu ya ugonjwa mwaka 2022 kwa mujibu wa Kifungu cha 32(1) cha Kanuni za Mitihani.

“Kati ya watahiniwa waliopewa fursa ya kurudia upimaji/mitihani yao mwaka 2022, watahiniwa 198 ni wa Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA) na 357 ni wa Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE).

Pamoja na mambo mengine amesema matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT) takwimu zinaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 4,763 sawa na asilimia 57.23 ya watahiniwa 8,324 wenye matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT) wamefaulu.

“Mwaka 2020 jumla ya watahiniwa 4,446 sawa na asilimia 55.19 walifaulu mitihani wa Maarifa (QT), hivyo ufaulu wa Mtihani wa Maarifa (QT) umepanda kwa asilimia 2.04,” amesema.

error: Content is protected !!