December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanafunzi 199 wa msingi Bukoba Vijijini wapata afueni

Kwon Yon Kag (mwenye kofia) akizindua jengo la madarasa mawili la shule ya sekondari Kasharu iliyopo kata ya Kasharu, Bukoba Vijijini, mkoani Kagera

Spread the love

JUMLA ya wanafunzi 199 wanaosoma darasa la VII kwa mwaka 2019 katika shule za msingi nne, zilizopo kwenye Kata ya Kasharu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijijini, wanatarajia kuondokana na adha ya kutembea urefu wa kilometa 16 kuifuata Shule ya Sekondari katika Kata ya Kishogo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kagera … (endelea).

Kwa kipindi cha zaidi ya miaka 11, wanafunzi katika Kata ya Kasharu wamekuwa wakitembea umbali huo jambo ambapo sasa adha hiyo inatarajia kuisha mara baada ya wanachi wa vijiji vya Kasharu, Kabajugana na Butainamwa kukabidhiwa vyumba viwili vya madarasa.

Akizungumza katika uzinduzi wa ujenzi wa vyumba hivyo vya awali, Twaha Issa ambaye ni ofisa elimu wa kata hiyo amesema kuwa, wanafunzi wanaomaliza darasa la saba wamekuwa na changamoto ya kuitafuta elimu ya sekondari maeneo ya mbali.

Amesema, vyumba hivyo vilijengwa kwa nguvu ya wananchi pia mfadhili kutoka nchini Korea ambaye alichangia vifaa mbalimbali ambavyo vimesaidia kuweza kukamilisha ujenzi wa vyumba hivyo. Tayari Sh. 35 Milioni zimetumika.

Ameeleza kuwa, kutokana na changamoto hiyo serikali ya kata na kijiji waliamua kuanza mara moja ujenzi huo kwa kukusanya michango kutoka kwenye jamii, ili waweze kuhakikisha watoto wanaomaliza darasa la saba mwaka 2019, wasipate adha ya mwendo mrefu.

Aidha, alibainisha kuwa, tayari shule ina ardhi kubwa kwa ajili ya ujenzi ambapo mmoja wa wanakijiji hicho Aloys Rwakatare ametoa eneo la ekari mame bure kuwa kiwanja cha shule.

Cosmas Barongo, Mwenyekiti wa Kijiji Kasharu amesema kuwa, kumekuwepo na tatizo kwa watoto wa kike wanaosoma mbali na kwamba, msaada huo ni mwokozi kwa watoto hao.

error: Content is protected !!