Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanafunzi 1300 kidato cha kwanza watokomea kusikojulikana, DC acharuka, atoa siku 7
Habari Mchanganyiko

Wanafunzi 1300 kidato cha kwanza watokomea kusikojulikana, DC acharuka, atoa siku 7

Spread the love

MKUU wa wilaya ya Mbozi mkoani Songwe Ester Mahawe ametoa siku  saba kwa maafisa elimu wilayani Mbozi kuhakikisha wanafunzi 1300 wa kidato cha kwanza mwaka huu ambao hawajaripoti shule wawe wameripoti. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Wilaya ya Mbozi ni moja ya wilaya kongwe nchini inayotegemea zao kuu la kahawa kama chanzo kikuu cha uchumi, lakini imekuwa na changamoto kadhaa za ufaulu mdogo kwa baadhi ya shule.

Mahawe aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika kikao cha kujadili mikakati ya kuongeza ufaulu wilayani humo baada ya kuripotiwa uwepo wa utoro uliokithiri kwa wanafunzi kwa baadhi ya shule hali iliyotajwa kuzidi kudidimiza jitihada za ongezeko la ufaulu.

‘’Rais Dkt,Samia,katika kipindi hiki cha utawala wake wa awamu ya sita, amefanya jitihada kubwa za kujenga madarasa shinikizi pasipo wananchi kuchangishwa, kazi kubwa ya wazazi ni kuhakikisha mtoto anaenda kusoma ambayo ni haki yake ya kimsingi,” alisema Dc Mahawe.

Agizo hilo la mkuu wa wilaya limekuja baada ya taarifa iliyowasilishwa na afisa elimu sekondari, Juma Tukosa,ambaye katika taarifa hiyo alisema wanafunzi 1300 waliotakiwa kuripoti kidato cha kwanza hawajaripoti toka mwezi Januari.

Afisa elimu huyo alisema ameyapokea maagizo ya mkuu wa wilaya na kuahidi kufanya jitihada za haraka kwa kushirikiana na wadau wa elimu kuhakikisha wanafunzi hao wanaripoti shule.

Edson Mdolo afisa mtendaji wa kata ya Ukwile alisema kuna sababu mbalimbali zinazofanya watoto hao kutoripoti shule ikiwemo baadhi yao kuishi na mama au bibi ambao hawana nguvu ya kumfuatilia mtoto kutokana na hali ya maisha waliyonayo.

Aidha, aliahidi kuwa wa kama watendajo wanaendelea na jitihada za kuhakikisha wanaripoti shule,

Frola Furaha mkazi wa Mbozi alisema agizo la mkuu wa wilaya linamashiko licha ya kuwa kuna changamoto kadhaa zinawakumba baadhi ya watoto ambao wanaishi na mzazi mmoja.

Aliongeza kuwa wazazi au walezi ndiyo wanaopaswa kulaumiwa kwa kutowafuatilia watoto licha ya serikali kujenga madarasa shinikizi katika kila shule.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!