Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Wanafunzi 1,143 wajitokeza mashindano ya tafiti za kisayansi
Elimu

Wanafunzi 1,143 wajitokeza mashindano ya tafiti za kisayansi

Mwanzilishi Mwenza wa Shirikisho la Wanasayansi Chipukizi (YST), Gozibert Kamugisha
Spread the love

 

ZAIDI ya wanafunzi 1143 wamejitokeza kuomba kushiriki mashindano ya gunduzi na tafiti za kisayansi yaliyoandiliwa na Shirikisho la Wanasayansi Chipukizi (YST) ambayo kitafa yanatarajiwa kufanyika Desemba 8, mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mashindano hayo yenu lengo la kuongeza chachu kwa wanafunzi kufanya tafiti za kisayansi kwa mwaka huu yanatarajiwa kufanyika mkoani Dar es Salaam huku mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwanzilishi Mwenza wa YST, Gozibert Kamugisha alisema jumla ya kazi za utafiti na kisayansi 530 zimepatiwa usaidizi ambapo wanafunzi walioziandaa wamepatiwa mafunzo ya namna ya kuziboresha na hatimaye kazi za kisayansi na ugunduzi 380 zimekamilika.

Alisema kazi za kisayansi na teknolojia zitakazoonyeshwa kwenye maonyesho ya mwaka huu zimejikita zaidi katika masuala ya njia salama za utunzaji wa mazao ya kilimo, mazingira na matumizi endelevu ya rasilimali ya maji, dawa za asili na uboreshaji afya za binadamu.

“Kazi zingine zitakazoonyeshwq ni upatikanaji na uzalishaji wa nishati ya umeme, matumizi ya muziki katika ufundishaji wa somo la hesabu shuleni, matumizi ya mimea ya asili katika kuboresha uzalishaji wa maziwa ya ng’ombe na kutatua tatizo la udumavu wa ukuaji wa kuku,” alisema.

Aidha alisema kazi zote hizo zilizojikita katika kupata njia za kutatua matatizo ya kimaendeleo zitaonyeshwa katika maonyesho ya kitaifa ya YST 2022. “YST imekua jukwaa la vijana kuonyesha ujuzi wao na kutoa fursa kwa wanafunzi kuvumbua njia z kisayansi kukabiliana na changamoto za kimaendeleo,”alisema na kuongeza.

“Walimu wa Sayansi na wanafunzi wamepatiwa mafunzo ya methodolojia za kisayansi kupitia mpango wa mafunzo ya ugunduzi na utafiti mashuleni umekuwa wa mafanikio na umeongeza hari na mwamko wa wanafunzi kujihusishà na sayansi na ugunduzi kwa kiasi kikubwa,”alisema.

Naye Ofisa Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Karimjee Jivanjee, Caren Rowland alisema shirika hilo limekuwa likiwafadhili YST kwa miaka 12 mfululizo ikiwa ni pamoja na kutoa udhamini wa elimu ya juu kwa wanafunzi wote washindi wa mashindano hayo pindi wanapomaliza masomo yao ya elimu ya huu.

Alisema hadi kufikia mwaka 2021 mpaka taasisi hiyo imeshawadhamini wanafunzi 37 huku wanne watakoshinda mwaka huu wataendelea kupewa ufadhili na idadi kufikia 41.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

ElimuMakala & Uchambuzi

Waraka maalumu kwa NECTA, “hawapaswi kuungwa mkono”

Spread the loveHATUA iliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), ya...

Elimu

NACTVET yafungua dirisha la udahili

Spread the love  BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo...

Elimu

Prof. Mwakalila awafunda wanafunzi Chuo Mwalimu Nyerere, “ulipaji ada ni muhimu”

Spread the love  MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere (MNMA),...

error: Content is protected !!