July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanachama CCM wamtwanga Katibu wao

Spread the love

HALI isiyokuwa ya kawaida wanachama na wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Bugogwa, Mwanza wamevamia na kumtembezea kichapo, Katibu wa chama hicho, wilaya ya Ilemela, Acheni Maulid, kwa madai ya kushindwa kurejesha jina la mshindi katika kura za maoni, Maliki Hatib. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Tukio hilo ni mwendelezo wa matukio ya aina hiyo kutokea katika wa kura za maoni ndani ya chama hicho, kilichogubikwa na vitendo vya vurugu na kupingwa matokeo.

Vurugu hizo zilimetokea jana saa tano asubuhi katika ofisi za CCM zilizopo eneo la Maliasili Pasiansi, wakati wanachama hao zaidi ya 30 walipoandama mpaka ofisini hapo kwa lengo la kutaka kufahamu chanzo na sababu za kukatwa kwa mshindi huyo.

Mwanahalisi Online, imeshuhudia wanachama hao wakitoa kichapo kwa katibu huyo, kwa ngumi na mateke huku wakimtoa nje ya ofisi kabla ya askari polisi kufika eneo hilo na kuzima vurugu hizo kwa kufyatua mabomu ya machozi.

Pamoja na polisi kupiga mabomu ya machozi, wanachama hao waliendelea kufanya fujo zilizodumu kwa saa nne, polisi walifanikiwa kumkamata mwanachama mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja.

Mwenyekiti wa UVCCM, Kata ya Bugogwa, January Samamba na Mwenyekiti wa Kata hiyo, Amos Samwel, kwa pamoja wamesema kitendo cha viongozi wa chama hicho kushindwa kurudisha majina ya watu wanaokubalika kutasababisha kishindwe katika uchaguzi wa mwaka huu.

Walidai kuwa kamwe hawatakubali kuona haki ya mtu ikipotea na wakafumba macho na kwamba endapo viongozi wa ngazi ya juu watalazimisha kupitisha jina la Steven Mashamba, ambaye alikuwa mshindi wa pili aliyepata kura 597, watapigia kura vyama vya upinzani.

“Kama watampishia huyo wanayemtaka wao kwa kisingizo kwamba, Hatib sio mtanzania, watampigia kura wao wenyewe sisi hatutapiga kura na tutawashawishi watu wengine kupigia upinzania,” wamesema wanachama hao.

Akizungumza na mara baada ya kutulia kwa fujo hizo, Katibu wa Wilaya hiyo, Acheni Maulidi, amesema chanzo cha kukatwa jina mshindi huyo ni kutokana na uraia wake kuwa shaka hivyo wasingeweza kumpitisha.

Amesema mara baada ya kura za maoni kumalizika na majina kupelekwa mkoani, walianza kuyapitia majina yote ambako mshindi huyo alitiliwa shaka na uraia wake na kumtaka kupeleka vyeti vya kuzaliwa na kwamba alishindwa kufanya hivyo.

Mshindi wa matokeo hayo, Maliki Hatib amesema kitendo cha viongozi wa CCM kushindwa kurudisha jina lake kitasababisha chama hicho kuacha kuchaguliwa na kuchukiwa na wananchi na kwamba yeye ni raia halisi wa Tanzania.

error: Content is protected !!