Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wamimilika uzinduzi kampeni za urais Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Wamimilika uzinduzi kampeni za urais Chadema

Spread the love

MAMIA ya wananchi wanaendelea kujitokeza katika uzinduzi wa kampeni za urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) zinazofanyika leo Ijumaa tarehe 28 Agosti 2020,  Uwanja wa Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Tundu Lissu ndiye anayepeperusha bendera ya Chadema kwenye nafasi ya urais na Salumu Mwalimu mgombea mwenza.

Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema bara na Mwalimu, naibu Katibu Mkuu-Zanzibar tayari wamewasili uwanja hapo.

          Soma zaidi:-

Ulinzi umeimarishwa katika viwanja hivyo, ambapo kuna baadhi ya askari polisi wa kawaida na wale wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU).

Pia, kuna walinzi maalum wa Chadema ambao wanafanya kazi ya kuongoza watu waliofika katika kampeni hizo.

 

Kampeni za Uchaguzi Mkuu zilifunguliwa rasmi tarehe 26 Agosti na zitahitimishwa tarehe 27 Oktoba 2020 ambapo kesho yake yaani Jumatano itakuwa ni siku ya uchaguzi.

Katika uchauzi huo, Lissu atachuana na wagombea wengine 14 akiwemo Dk. John Magufuli, mgombea wa Chama cha Cha Mapinduzi (CCM), Prof. Ibrahim Lipumba (CUF), Yeremia Maganja (NCCR-Mageuzi).

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV ambao tuko live Youtube na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!