Saturday , 2 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Wamiliki Kunduchi Islamic wachunguzwa kwa rushwa
Habari Mchanganyiko

Wamiliki Kunduchi Islamic wachunguzwa kwa rushwa

Afisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani
Spread the love

 

TAASISI ya Munazzamat Dawa Al Islamiya (MDI) inayomiliki Shule ya Sekondari ya Kiislam ya Wasichana Kunduchi (Kunduchi Girls), inachunguzwa kwa tuhuma za rushwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam .. (endelea).

Taarifa ya uchunguzi huo imetilewa leo Jumanne tarehe 9 Machi 2021, na Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), Doreen Kapwani kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo, Brigedia Jenerali, John Mbugo.

Taarifa ya Kapwani imesema, katika uchunguzi huo, Takukuru imemhoji Mkurugenzi wa MDI, Ally Magoga na walalamikaji pamoja na kukusanya baadhi ya vielelezo vya ushahidi.

Taarifa ya Kapwani imesema, uchunguzi huo umeanzishwa baada ya Takukuru kupokea malalamiko kuhusu tuhuma mbalimbali inazokabili shule ya taasisi hiyo.

“Bila shaka baadhi yenu mlisikia na kuona malalamiko ya baadhi ya wazazi na wanafunzi wa shule hiyo ambayo yalirushwa katika Taarifa ya Habari ya Kituo kimoja cha Televisheni hivi karibuni yakiulalamikia uongozi wa Shule kwamba pamoja na mambo mengine imekuwa ikishindwa kuwalipa mishahara na posho nyingine, walimu na wafanyakazi wa shule hiyo,” imedai taarifa hiyo.

Miongoni mwa tuhuma hizo, ni, viongozi wa Shule pamoja na Bodi ya Wadhamini kufanya miamala ya fedha isiyo na uwazi, kushindwa kulipa fedha za walimu kiasi cha Sh. 406 milioni, kukwepa kulipa kodi ya serikali.

“Viongozi wa shule ikiwemo Bodi ya Wadhamini ya Shule inalalamikiwa kwa kusababisha madeni kwa walimu na wafanyakazi wa shule hiyo ambapo inadaiwa kwamba hadi kufikia mwezi Machi 2021, walimu na wafanyakazi wa shule ya Kiislamu ya Kunduchi wanaidai taasisi ya MDI kiasi cha Sh. 406 milioni ambayo Mkurugenzi wake hajataka kuwalipa,” imesema taarifa hiyo.

Tuhuma nyingine ni “Lalamiko lingine ni uongozi wa MDI kukwepa kulipa kodi halali za Serikali na hivyo kuisababishia Serikali hasara na kwamba mapato ya shule yamekuwa yakiishia mikononi mwa wajanja wachache ndani ya taasisi ya MDI.”

Katika tuhuma nyingine, mkurugenzi wa MDI anadaiwa kukodisha shule hiyo kinyume na utaratibu, akishirikiana na mkurugenzi wa elimu wa shule ya Kunduchi.

“Lalamiko lingine ni kwamba, Mkurugenzi wa MDI akishirikiana na Mkurugenzi mpya wa Elimu wa Shule ya Kunduchi wamekuwa wakiingia mikataba mibovu ya kuikodisha shule hiyo kwa wamiliki mbalimbali bila kufuata utaratibu,” imesema taarifa ya Kapwani.

Pia, MDI inatuhumiwa kuendesha Bodi ya Wadhamini ya shule hiyo tangu 2017, bila katika Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo ( RITA)

“Kwamba Bodi hiyo ya Wadhamini kwa kushirikiana na viongozi wa MDI, wamejipa mamlaka ya kuidhinisha malipo yote ya akaunti ya shule , jambo ambalo ni kinyume na utaratibu,” imesema taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari Mchanganyiko

Waziri Bashungwa aagiza wahandisi kujengewa uwezo

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili wa...

Habari Mchanganyiko

Heche ataka mawakili vijana kuamka sakata Mpoki

Spread the loveMWENYEKITI wa Mawakili Vijana Tanzania kutoka Chama cha Mawakili wa...

error: Content is protected !!