Monday , 29 May 2023
Home Kitengo Michezo Wambura ang’olewa Bodi ya Ligi, apewa ulaji TFF
Michezo

Wambura ang’olewa Bodi ya Ligi, apewa ulaji TFF

Boniface Wambura, Mkuu wa Habari na Masoko wa TFF
Spread the love

ALIYEKUWA Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amemaliza mkataba wake na amepewa kazi nyingine ndani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Masoko ambapo atasaidiwa na Clinford Ndimbo na Aron Nyanda. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Katibu mkuu wa TFF, Wilfred Kidau amesema kuwa baada ya Wambura kumaliza mkataba wake kama muajiliwa ndani ya Bodi ya Ligi, Kamati ya Utendaji imeamua kumrudisha ndani ya Shirikisho kwa kuwa bado anauwezo mkubwa wa kuhudumu katika nafasi hiyo ya habari na masoko ili kuongeza ufanisi. 

“Rais wa TFF, Walace Karia kwa kushirikiana na kamati tendaji wameamua kumteuwa Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Masoko akisaidiwa na Ndimbo kwenye upande wa habari na Aron Nyanda upande wa masoko ili kuongeza ufanisi katika shughuli za kila siku ndani ya shirikisho,” alisema Kidau.

Katibu aliendelea kusema kuwa nafasi ya mtendaji mkuu wa bodi ya ligi itatangazwa hivi karibuni kupitia vyombo vya habari.

Katika hatua nyingine Kamati ya utendaji imemteuwa Oscar Milambo kuwa Mkurugenzi wa Ufundi ya TFF akiziba nafasi iliyoachwa wazi na Ammy Ninje ambaye amerejea masomoni hivi karibuni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

NBC Dodoma Marathon yazinduliwa, wakiambiaji 6,000 kushiriki

Spread the loveBENKI ya NBC imetangaza kufanyika kwa mbio kubwa za NBC...

Michezo

Rais Samia anunua tiketi 5000 Yanga vs USM Alger

Spread the loveRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu...

Michezo

Mwenyekiti UVCCM anogesha nusu fainali Kimwanga CUP, Hawa Abdul Rede CUP kwa kishindo

Spread the loveHEKAHEKA za michuano ya kuwania kuingia fainali ya michuano ya...

Michezo

Yanga SC. yatwaa ubingwa wa pili mfululizo

Spread the love  KLABU ya Yanga SC imeweka rekodi ya kutwaa ubingwa...

error: Content is protected !!