Wednesday , 27 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Wamarekani wamwaga vyandarua kwa wajawazito Mwanza
Habari Mchanganyiko

Wamarekani wamwaga vyandarua kwa wajawazito Mwanza

Spread the love

WAJAWAZITO nchini wametakiwa kuwa na utamaduni wa kupima afya zao na kuhakikisha wanapata chanjo ya ugonjwa wa malaria ili kujikinga wao pamoja na watoto walipo tumboni, anaandika Moses Mseti.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi, wakati wa kugawa vyandarua kwa wanafunzi wa shule ya msingi Sese katika kata ya Bujashi wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Msaada huo umetolewa na wajumbe wa Bunge la Marekani wa masuala ya afya ambao waliotembelea shule hiyo.

Dk. Subi amesema tafiti za mwaka 2012 zinaonesha kuwa mkoa wa Mwanza asilimia 19 ya watu wake wanaugua ugonjwa wa Malaria, ikilinganishwa na asilimia 15 kwa mwaka 2015/ 2016.

Amesema kuwa wajauzito wanapaswa kupata chanjo pindi ili kuwasaidia kujikinga na ugonjwa huo.

“Mpango wa kugawa vyandarua ni wa taifa zima, lakini kwa mkoa wa Mwanza tumegawa vyandarua 50, 000 kwa akina mama wajawazito pindi wanapoanza kliniki yao ya kwanza na kinga ya mtoto chini ya miaka 15 ni hafifu inashauriwa kufika hospitali mapema”.

“Mkoa wetu tunatoa chanjo za kutosha za ugonjwa wa malaria kwenye hospitali zetu zote za mkoa wa Mwanza na zaidi ya dozi tatu ya ugonjwa huo hutolewa bure,” amesema Dk. Subi.

Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka ofisi ya Rais wa Marekani kitengo cha Malaria cha USAID, Chris Thomas amesema lengo lao ni kuhakikisha wanapunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa wa malaria hususani kwa akina mama wajawazito na watoto wadogo chini ya miaka 15.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari Mchanganyiko

Wizara ya madini kurusha ndege ya utafiti wa madini Geita

Spread the loveKutokana na mchango wa wachimbaji wadogo wa madini kwenye pato...

Habari Mchanganyiko

Jafo aagiza kampuni za madini kuzingatia utunzaji mazingira, azitaka zijifunze kwa GGML

Spread the loveWAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Spread the loveWANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk....

error: Content is protected !!