January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Walivyosema kuhusu Komba

Baadhi ya viongozi waliohudhuria msiba wa Komba

Spread the love

VIONGOZI mbalimbali wa kisiasa, wameungana na familia, ndugu na jamaa, kuomboleza kifo cha Mbunge wa Mbinga (CCM), John Damian Komba, aliyefariki dunia Jumamosi, 28 Februari 2015. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Maombolezo hayo yanafanyika nyumbani kwa marehemu, Tegeta, Tangibovu, wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Yafuatayo ndiyo yaliyosemwa na waombelezaji.

Anne Makinda, spika wa Bunge la Jamhuri:

“Komba alikuwa muwazi, mcheshi na alisema bila hofu. Nilikuwa mtu wa kwanza kumshauri agombee ubunge katika jimbo aliloliongoza. Sisi sote hatujui, mauti hufika ghafla. Siri ya Mungu ni kubwa.”

Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa:

“…tumempoteza kiongozi mashuhuli kwenye chama, taifa hata kimataifa. Tumempoteza mpiganaji aliyetekeleza kile alichokiamini. Msiba huu, ni mkubwa sana.”

Alisema, “kifo chake kinatufundisha kuwa sisi ni binadamu, muda wowote tunaweza kufa. Kwa sasa, ni muhimu kuiombea familia yake na kuisaidia.”

Joshua  Nassari, mbunge wa Chadema katika jimbo la Arumeru Mashariki. Yeye alisema yafuatayo:

“Nimepokea kifo cha Komba kwa msituko mkubwa. Kama mbunge mwenzangu na mjumbe mwenzangu katika Kamati ya Maendeleao ya Jamiii, tulikuwa na utofauti mkubwa wa itikadi katika siasa, lakini bado tuliweza kufanya kazi pamoja kwa maslahi ya taifa.

“Nawapa pole familia yake,wasanii wenzake,  CCM na wapigakura wake.”

Asha-Rose Migiro, mbunge wa kuteuliwa na waziri wa Katiba na Sheria.

“Kifo cha Jonh Komba ni pigo kubwa sana. Jimboni kwake walimuita wamyaya (wa maisha). Sisi wabunge kila mtu anaufahamu mchango wake alipokuwa bungeni. Alikuwa rafiki yangu. Nilionana nae siku mbili zilizopita. Tutamkubuka kwa ucheshi wake. Alikuwa na kipaji kikubwa cha sanaa.”

William Ngereja, mbunge wa Jimbo la Sengerema (CCM) amesema yafuatayo:

“Komba alikuwa mchapa kazi. Alijitoa. Amekuwa ni mtu wa kusema kweli kwa mambo anayoyaamini. Ameishi katika yeye. Kupitia kipaji chake, alionesha uzalendo. Hakika tutakosa kipaji ambacho Mungu alimjalia. Tunapaswa kujifunza yale yote mema aliyoyatenda.”

Dk. Stephen Kembwe, mbunge wa Serengeti (CCM).

“Alipenda utani wa kisisa. Alikuwa mhamasishaji mkubwa katika chama. Elimu yake haikuwa na itikadi.”

Amedai kuwa Komba alikuwa akihimiza wananchi kuwa na mshikamano, amani na utulivu.

Hata hivyo, Komba alikuwa miongoni mwa wabunge wa Bunge Maalum la Katiba, waliotishia kuingia msituni ikiwa Katiba yenye muundo wa serikali tatu, ingepitishwa bungeni.

Alimtuhumu Jaji Joseph Warioba, aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kuwa ni kibara wa nchi za magharibi.

error: Content is protected !!