December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waliouawa kanisani Sri Lanka wafika 290

Spread the love

MIILI ya watu waliopoteza maisha katika shambulio la kigaidi kwenye makanisa matatu na hoteli za kifahari nchini Sri Lanka, imefikia 290. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Shambulizi la mabomu katika makanisa yaliyoko Negombo, Batticaloa na Wilaya ya Colombo Kochchikade pamoja na hoteli za Shangri-La, Kingsburry na Common Grand yalitokea wakati wa ibada ya Sikuu ya Pasaka majira ya asubuhi jana tarehe 21 Aprili 2019.

Vyombo vya Habari vya Kimataifa vimeripoti kwamba, takribani watu 500 wamejeruhiwa kwenye shambulio hilo, na kwamba Jeshi la Polisi linawashikilia watu 24 wanaoshukiwa kuhusika na tukio hilo.

Taarifa za vyombo hivyo zinaeleza kwamba, mamlaka nchini Srilanka viliarifiwa wiki mbili kabla taarifa za tishio la kiusalama.

Katibu wa Masuala ya Ulinzi SriLanka, Hemasari Fernando amewataka wananchi wa taifa hilo kutovilaumu vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutozuia shambulizi hilo, akisema kwamba licha ya uwepo wa taarifa za matishio ya kiusalama, vyombo hivyo havikudhania kama magaidi wangetekeleza katika maeneo hayo.

error: Content is protected !!