SIKU moja tangu Rais Samia Suluhu Hassan aengue mawaziri na naibu mawaziri kutoka Baraza lake, wamemshukuru wakisema, hawawanii urais na au kuunga mkono wanaouwania katika uchaguzi mkuu mwaka 2025. Anaripoti Ibrahim Yamola…(endelea).
Katika mabadiliko ya Baraza hilo yaliyotangazwa juzi, Rais Samia aliwaweka kando mawaziri wanne na naibu mawaziri wawili, ikiwa ni takribani wiki moja tangu alipotangaza mabadiliko hayo.
Rais Samia alisema, mabadiliko hayo yanalenga kuwaweka kando walioanza harakati za kusaka urais, au wanaowaunga mkono katika uchaguzi mkuu wa 2025 ili wakajiandae vizuri.
Mawaziri walioachwa na wizara zao kwenye mabano; ni Profesa Palamagamba Kabudi (Katiba na Sheria), Geoffrey Mwambe (Uwekezaji), William Lukuvi (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) na Profesa Kitila Mkumbo wa Viwanda na Biashara.
Naibu mawaziri ni Mwita Waitara wa Ujenzi na Uchukuzi na Profesa Shukuran Manya wa Madini.
Tumezungumza na baadhi yao, Waitara na Profesa Manya.
Nini wamekisema, soma gazeti la Raia Mwema la leo Jumatatu, 10 Januari 2022.
Leave a comment