February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waliotoroka Mgambo wapewa siku mbili kurudi kambini

Spread the love

VIJANA takribani 200 waliotoroka katika mafunzo ya mgambo wapewa saa 48 ambayo ni sawa na siku mbili kurudi kambini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Agizo hilo limetolewa mapema leo tarehe 1 Oktoba 2018 na Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mhandisi Zephania Chaula wakati akifungua mafunzo ya mgambo katika kijiji cha Terrat mkoani Arusha.

Pia, Mhandisi Chaula amewaagiza wenyeviti wa vijiji na vitongoji kwa kushirikiana na watendaji wa kata kusimamia utekelezwaji wa agizo hilo ili vijana hao warudi kwa ajili ya kuendelea na mafunzo.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Chaula amewataka vijana wanaoendelea na mafunzo ya mgambo kuzingatia mafundisho yao ili baadae wawe tegemeo kwa taifa katika shughuli za ulinzi na usalama.

error: Content is protected !!