March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Walioshikilia Bombadier wamlima barua JPM

Spread the love

KAMPUNI ya mawakili nchini Canada – Irving Mitchell Kilichman (IMK) – imemlima barua Rais John Magufuli, iliyosheheni masharti mazito ya kuachiwa ndege yake aina ya Bombadier Q400, anaandika Saed Kubenea.

Taarifa kutoka Ikulu, jijini Dar es Salaam, wizara ya mambo ya nje na ubalozi wa Tanzania nchini Canada zinasema, IMK imechukua hatua hiyo, kufuatia maelekezo iliyopewa na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd (SCEL) ya nchini humo.

SCEL inadai serikali ya Tanzania kiasi cha dola za Marekani 38.7 milioni (Sh. 87 bilioni), kufuatia kuvunjwa kwa mkataba wake wa ujenzi wa barabara ya Dar es Salaam hadi Bagamoyo, miaka 13 iliyopita.

Katika barau hiyo, SCEL inasema, haitaachia ndege ya Tanzania inayoishikilia mpaka serikali ilipe kwanza dola milioni 12.5 (sawa na bilioni 27.8) kati ya dola 38.7 inazopaswa kulipa.

Aidha, SCEL inasema, haitaachia ndege hiyo mpaka Rais Magufuli na serikali yake, watakapokubali kwa maandishi, kulipa kiasi kingine cha dola za Marekani 25.5 milioni.

Habari kamili juu ya taarifa hiyo, soma gazeti la MwanaHALISI la leo (Jumatatu).

error: Content is protected !!