Friday , 24 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Walioshika mkia ukusanyaji mapato 2017/18 wapewa agizo zito
Habari Mchanganyiko

Walioshika mkia ukusanyaji mapato 2017/18 wapewa agizo zito

Suleiman Jafo, Waziri wa Tamisemi
Spread the love

WAZIRI wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jaffo, amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela John Wanga, kuongeza jitihada na juhudi za ukusanyaji wa mapato ili kuondoa aibu ya manispaa hiyo iliyoshika mkia kwenye ukusanyaji wa mapato nchini. Anaripoti Moses mseti, Mwanza … (endelea).

Jaffo ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na watumishi katika halmashauri hiyo, na kumtaka Wanga pamoja na watendaji wa manispaa hiyo kubadilika na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Waziri Jaffo alisikitishwa na kumlazimu kuuliza sababu za halmashauri hiyo kushindwa kufikia malengo yao ya Sh. 11 bilioni na kusababisha kuwa ya mwisho kwenye ukusanyaji wa mapato katika bajeti ya mwaka 2017/18.

Baada ya swali la Jaffo kwa mkurugenzi wanga, Mchumi wa Halmashauri hiyo, Amos Zephania alinyanyuka na kusema, walishindwa kukusanya fedha hizo kutokana na mabadilo ya kimfumo.

Kufuatia kauli hiyo, Jaffo aliwataka na kuwahimiza watendaji hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea huku akidai kutofanyika marekebisho kwenye mfumo kwa wakati ni uzembe wao wala si vinginevyo.

“Nakuomba Mkurugenzi (John Wanga) usiwaonee aibu watendaji wako, wewe timiza wajibu kwa kuwasimamia ipasavyo, badala yake aibu hiyo itakugeukia wewe, maana wakivurunda wao ni wewe unakuwa umevurunda,” alisema Jafo

Alisema katika halmashauri hiyo bado kuna watendaji ambao bado ni wazembe ambao wanakwamisha ukusanyaji wa mapato kwa halmashauri hiyo.

“Nyie mlichokipata ni aibu kwenu mkurugenzi, lazima watumishi tubadilike watu wanafanya kazi kwa mazoea na hatutamvulia mtumishi yeyote,” aliongeza Jaffo.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, John Wanga alisema atahakikisha anasimamia maelekezo hayo na kuhakikisha kila mtendaji anatimiza wajibu wake.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo alitembelea na kukagua jengo la utawala la manispaa hiyo ambalo linagharimu Sh3.8 bilioni, ujenzi wa jengo la dharura la hospitali ya Wilaya ya Ilemela linalogharimu Sh. 769 milioni na vituo vya afya vya Buzuruga na Igoma vinavyogharimu Sh. 400 kila kimoja.

Akiwa katika kituo cha Igoma Waziri Jaffo alikiri kuridhishwa na ujenzi wa kituo cha afya Igoma na kuwapongeza watendaji wa halmashauri ya jiji la Mwanza chini ya Mkurugenzi wake Kiomoni Kibamba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko awataka makatibu mahsusi kujiendeleza, kuwa kielelezi cha huduma bora

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

GGML inavyookoa walemavu dhidi ya dhana potofu

Spread the loveMKOA wa Geita ni mmoja wa mikoa ya Kanda ya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Tanzania kufungua vituo 100 vya kufundisha Kiswahili nje

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania imepanga kufungua vituo 100 vya kufundisha lugha...

Habari MchanganyikoTangulizi

11 wafariki dunia baada ya mtambo wa Kiwanda cha Mtibwa Sugar kupasuka

Spread the loveWATU 11 wamefariki dunia huku watatu wakijeruhiwa katika ajali ya...

error: Content is protected !!