Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Walioporwa fedha kwenye mabenki kurejeshewa
Habari MchanganyikoTangulizi

Walioporwa fedha kwenye mabenki kurejeshewa

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba
Spread the love

 

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema fedha zilizochukuliwa kimakosa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), katika akaunti za benki, zitarejeshwa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Mwigulu ametoa kauli hiyo akizungumza katika mahojiano yake na Kituo cha Televisheni cha Azam TV, leo tarehe 9 Julai 2021.

Waziri huyo wa fedha amesema, fedha hizo zitarejeshwa endapo Serikali itabaini zilichukuliwa kimakosa.

“Nawasihi waende katika ofisi husika na uamuzi utafanyika, lazima reconciliation (upatanisho) ufanyike, huwezi sema kwenye blanket wote waliochukuliwa fedha kwenye akaunti zilizofunguliwa warejeshewe,” amesema Dk. Mwigulu.

Dk. Mwigulu amewataka watu hao wafike katika ofisi za TRA, wakiwa na vielelezo vinavyoonesha taarifa zao za fedha na kodi wanazodaiwa.

“Kama kuna mtu ana jambo mahsusi afike ofisi moja ya TRA, aseme namba zinasema hivi na kama hajaridhika Serikali yetu ina check and balance. Ofisi zetu ziko wazi tunasikiliza malalamiko ya aina hiyo,” amesema Dk. Mwigulu.

Dk. Mwigulu ameongeza “nadhani hilo liwe namna hiyo, sababu haliwezi kuwa kwenye mstari mmoja, anaweza mtu kodi yake imechukuliwa kimakosa hata asipopewa cash (taslimu), atapewa kwa mfumo mwingine.”

Alphayo Kidata, Kamishna Mkuu wa TRA

Amesema, kama mhusika ni mfanyabiashara fedha zake zilichukuliwa kimakosa, zitarudishwa kwa mfumo wa kumlipia kodi, kulingana na kiwango cha fedha zake.

“Hata asipolipwa cash, mwezi huu inakatwa ile iliyotumika kimakosa. Kama kuna makosa yalifanyika ya kimahesabu, wafike kwenye ofisi zetu kufanya mahesbau na kama hajaridhika waje kwenye ofisi nyingine ziko wazi,” amesema Dk. Mwigulu.

Sakata la fedha kuporwa ndani ya akaunti za benki, liliibuka baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuagiza akaunti zilizofungwa zifunguliwe, ambapo baadhi ya wamiliki wake walikuta fedha hazipo.

Akitolea ufafanuzi suala hilo, Dk. Mwigulu amesema akaunti nyingi zilizofungwa zilikuwa na migogoro ya kikodi na kwamba sio fedha zote zilichukuliwa kimakosa.

Kwa kuwa baadhi ya wamiliki wake walikuwa wanadaiwa kodi nyingi, ikilinganishwa na fedha hizo.

“Maeneo mengi ambayo akaunti ilishikiliwa kulikuwepo mizozo ya kikodi, maeneo mengi fedha iliyokuwepo ni ndogo kuliko kodi inayodaiwa sababu kulikuwepo na malimbikizo ya kodi,” amesema Dk. Mwigulu na kuongeza:

“Rais aliekeza kwamba hata anayedaiwa afunguliwe akaunti aendelee kuzalisha na kufanya kazi ili fedha inayopatikana iendelee kutengeneza kodi zingine.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

error: Content is protected !!