
Uwanja wa Ndege wa Mpanda baada ya upanuzi
SERIKALI imekamilisha ulipaji wa fidia kwa wananchi waliopisha upanuzi wa ujenzi wa viwanja vya ndege Mpanda katika mkoa wa Rukwa. Anaandika Dany Tibason … (endelea).
Kauli hiyo ilitolewa bungeni na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri, Tamisemi Aggrey Mwanri, ambaye amesema kuwa Serikali ilitwaa baadhi ya maeneo hayo katika kipindi cha mwaka 2011 kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa kiwanja cha ndege katika mji wa Mpanda.
Mwanri akijibu swali la mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi (Chadema), ambaye alitaka kujua kama ni utawala bora kwa wananchi wa Mpanda waliopisha ujenzi wa uwanja wa ndege ambao wamekosa baadhi ya huduma kama barabara na maji.
Mbunge huyo alitaka kujua ni hatua gani zimefikiwa za kuondoa kero hiyo baada ya tume kufika na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo husika.
Naibu Waziri alisema ili kutekeleza azma hiyo, Serikali ilitwaa maeneo ya wananchi ili kuwa na eneo la kutosha kwa ajili hiyo na upanuzi huo ulihusisha maeneo ambayo hayakuwa maalumu kwa ajili ya makazi ya watu kuishi.
“Kuhusu kuondoa kero kwa wananchi waliokuwa kwenye maeneo yao kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege ambako Mkuu wa wilaya aliunda tume ya kusimamia na kuhakikisha haki inatendeka kwa kila mwananchi kulipwa fidia stahiki,” amesema Mwanri.
Amesema hatua zingine zilizochukuliwa ni ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilimota 1.5 kwa gharama ya sh 30 milioni katika eneo la Airtel lililoko katika Kata ya Nsemulwa na ujenzi wa mradi wa maji wa Ikorongo ambao unavituo viwili vya kuchotea maji.
More Stories
Mapadri 25, Masista 60 waaga dunia Tanzania
TCRA yajitosa bei za vifurushi
Huawei yaunga mkono malengo endelevu UN