July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waliopisha ujenzi kulipwa mil. 281/-

Askari wa Usalama barabarani akiwa kazini

Spread the love

SHILINGI 281.5 milioni, zitatumika kuwalipa fidia wananchi 55 walioathirika na ujenzi wa barabara ya Arusha – Namaga, Serikali imesema.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge ametoa kauli hiyo bungeni alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Arumeru Magharibi, Godluck ole Madeye (CCM).

Katika swali la msingi la mbunge huyo, alitaka kujua ni lini wananchi wa Oldonyosambu na Mateves watalipwa fidia kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha sheria ya barabara namba13 ya mwaka 2007.

Katika majibu yake, Mhandishi Lwenge, amesema kuwa barabara ya Arusha-Namanga ni kuu inayohudumiwa na wizara husika kupitia Wakala wa Barabara nchini.

Ameongeza kuwa, barabara hiyo imekuwepo tangu enzi za ukoloni na inatambuliwa na sheria ya barabara CAP,167 ya mwaka 1967 na mabadiliko yake kupitia sheria Na. 13 ya mwaka 2007.

Kwa mujibu wa Lwenge, mali za wananchi wa kijiji cha Oldonyosambu zilizoathiriwa wakati wa ujenzi wa barabara ya Arusha Namanga zilifanyiwa tathmini.

“Jumla ya Sh. 281.5 milioni zinahitajika kulipa fidia kwa wananchi 55 ambao ndio waathirika. Serikali haima mpango wa kuwalipa fidia wananchi wa kijiji cha Mateves kwa kuwa wao hawakuguswa na tatizo hilo.

error: Content is protected !!