July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waliopisha ujenzi bandari kavu kulipwa fidia

Kigoma Ujiji

Spread the love

WIZARA ya Uchukuzi imekiri kuwa na fedha za kulipa fidia kwa wananchi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji lakini tatizo ni kwa wahusika kutokukamilisha taratibu za kibenki, bunge limeelezwa leo. Anaandika Dany Tibason …. (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi Dk. Charles Tzeba ambaye amesema  kuwa taratibu za wananchi hao zikikamilika watalipwa wakati wowote.

Alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum, Sebreena Sungura (Chadema), ambae alitaka kujua ni katika bajeti ya mwaka gani wananchi wa eneo la Butungu/Katosho katika Manispaa ya Kigoma Ujiji watalipwa fidia ili kupisha mradi wa Bandari Kavu katika eneo hilo.

Mbunge huyo pia alilalamikia viwango vya ulipaji wa fidia ambavyo zimekuwa vikifanywa na watumishi kwa madai ya kuwapunja wananchi na kuwafanya wasshindwe hata kununua viwanja vya kujenga.

Naibu Waziri amesema  tathimini ya utwaaji wa eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 69 kwa ajili ya ujenzi wa bandari kavu ilikamilika mwaka 2013 na baadhi ya watu walishalipwa stahiki zao.

“Tathimini ilibaini kuwa jumla ya Sh 12.043 bilionizinahitajika kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wakazi 1,228 watakaopisha eneo la mradi  huo wa ujenzi,” amesema Tzeba.

Amesema  Serikali kupitia Mamlaka ya usimamizi wa bandarai Tanzania (TPA), ilianza kulipa fidia kwa wakazi wa eneo hilo April 2015 na hadi kufikia Juni 15, 2015, jumla ya wakazi 1,135 walishalipwa.

Aidha,amesema thamani ya fidia iliyolipwa ni sh 10.1 bilioni na kwamba fidia kwa wakazi 93 waliobaki watalipwa wakati wowote baada ya wao kukamilisha taratibu za kibenki.

error: Content is protected !!