December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waliopata ujauzito kurudi shule

Mwanafunzi mjamzito

Spread the love

 

SERIKALI imesema imeamua kuondoa vikwazo vya elimu hususani kwa wasichana ambao wamekatisha masomo yao kwa kukumbwa na matatizo mbalimbali ikiwamo kupata ujauzito. Anaripoti Danson Kaijage- Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mafanikio na changamoto za wizara hiyo katika kipindi cha miaka 60 iliyopita.

Prof. Ndalichako amesema serikali imeamua kuondoa vikwazo vya elimu kwa watoto ambao wanakumbana na changamoto zilizokatiza masomo yao.

Amesema wapo baadhi ya watoto ambao wanashindwa kumaliza masomo na kukosa fursa ya kupata elimu jambo ambalo litaathiri maisha yao.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako

“Tunajua wapo baadhi ya watoto ambao wamepata ujauzito, serikali imeamua kwamba wanapokuwa tayari… watarudi darasani na watafanya mitihani kama kawaida na wakifaulu watapangwa katika shule za serikali” amesema Prof. Ndalichako.

Neema hiyo pia inawaangukia hata vijana wa kiume ambao wamekatiza masomo yao hivyo watakapokuwa tayari ndani ya miaka miwili wataweza kuendelea na masomo yao na watakapokuwa wamefaulu watapangwa katika shule za serikali.

Sambamba na hilo Prof. Ndalichako amesema kuwa hata wale ambao walifutiwa matokeo ya mitihani wanayofursa ya kurudia mitihani kwa lengo la kutoikosa fursa hiyo muhimu.

error: Content is protected !!