January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waliopata mimba za utotoni kurudi shuleni

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imeandaa mikakati ya kuwarudisha mashuleni wanafunzi wa kike walioathilika kwa kupewa mimba za utotoni na kuwachukulia hatua wote wanaojihusisha na kufanya ukatili wa kijinsia kwa wasichana hao. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Paulina Mkonongo katika uzinduzi wa maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, uliofanyiika katika ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

Paulina akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzi ya Ufundi, Sifuri Mchome katika uzinduzi huo.

Akisoma hotuba maalimu kwa niaba ya mgeni rasmi, baada ya maandamano kutoka viwanja vya Tipi, Tandale Darajani- Ubungo Plaza, Mkonongo amesema kuwa utafiti unaonyesha kuwa watu wenye mamlaka ya kuwalinda watoto ndio wanaohusishwa na unyanyasaji wa kijinsia ambapo wenye mamlaka hayo ni pamoja na wazazi, walezi na hata walimu mashuleni.

Kwa mujibu wa sera ya elimu ya mwaka 2014, takwimu za mwaka 2012 zinaonyesha wasichana 31,437 kati ya wanafunzi 8,247,172 waliacha shule kutokana na sababu mbalimbali huku mimba za utotoni zikitajwa kuwa chanzo kikubwa cha wasichana hao kushindwa kuendelea na masomo.

Mkonongo amesema kuwa wanawake pamoja na watoto ni miongoni mwa wanaoathilika kisaikolojia kutokana na wao kuwa tofauti na wanaume hivyo hatua ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia nchini humo ni muhimu kimaendeleo ya nchi.

Maadhimisho hayo yataadhimishwa nchini siku 16 katika mikoa mbalimbali kwa njia tofauti pamoja na kuchangisha ada kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu, pamoja na kuonyesha filamu mbalimbali za kuelimisha kuhusu kupinga ukatili wa kijinsia.

error: Content is protected !!