Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa shule hiyo, Gladius Ndyetabura wakati akizungumza na gazeti hili kuhusu matokeo ya kidato cha nne ambapo wanafunzi 103 wa shule hiyo walifanikiwa kupata daraja la kwanza.
Alisema kwenye mtihani huo wanafunzi 40 walipata daraja la pili na wanafunzi saba pekee ndio wamepata daraja la tatu.
“Haya ni matokeo mazuri sana kwetu ukizingatia tulikuwa na wanafunzi wengi lakini wote wamefanikiwa kupata nafasi ya kuendelea na kidato cha tano ndiyomaana tunawaandalia safari hii ya kwenda Mikumi na Ngorongoro kama motisha kwao na kwa wenzao ili wapate ari ya kufanya vizuri,” alisema
Aliwapongeza na kuwashukuru walimu wa shule hiyo ambao wamefanyakazi kubwa usiku na mchana kuhakikisha wanafunzi wote wanafaulu kwa ufaulu wa juu na alimshukuru pia Mkurugenzi wa shule hiyo, Dk. Jasson Rweikiza kwa ushirikiano ambao amekuwa akiutoa kwa walimu.
Alitaja siri ya mafanikio hayo kuwa ni shule kuwa na mazingira mazuri ya wanafunzi kusomea ikiwemo maktaba ya kisasa na maabara iliyosheheni vifaa vya kutosha pamoja na walimu mahiri wanaojua kazi yao
“Wanafunzi wetu wanakula milo minne kwa siku na tuna mashamba ya mboga mboga na matunda kwa hiyo wanakula mlo kamili na mazingira kwa ujumla ni mazuri sana kuwawezesha kujisomea muda wowote,” alisema
Alisema shule hiyo imedhibiti ulinzi kwa kuweka walinzi 46 wenye mafunzo wakisaidiwa na mbwa wao ambao wamekuwa wakizunguka usiku na mchana kuhakikisha kunakuwa na usalama.
“Hawa walinzi wetu wamepata mafunzo ya kisasa kiasi kwamba hata ukitokea moto wakotayari kuuzima ndani ya dakika chache kwa hiyo wazazi msiwe na wasiwasi kuhusu taaluma na suala la usalama,” alisema
Mwaka 2021 St Anne Marie Academy ilitoa mwanafunzi bora kitaifa, Elulei Haule anayesoma kidato cha kwanza shule ya Marian Boys ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Akizungumza kwenye mahafali ya kidato cha nne mwaka huu, Mkurugenzi wa shule hiyo, Dk. Rweikiza, alitangaza kwamba hakuna mwanafunzi yoyote wa shule hiyo atakayefukuzwa kwasababu ya kufiwa na wazazi wake na kukosa ada.
Alisema wakati wa mlipuko wa korona mtandao wa shule zake ulipoteza wazazi 46 lakini hakuna aliyewahi kufukuzwa kwa kushindwa kulipa ada na wanaendelea.
“Nilisema wakati ule tulipopoteza wazazi 46 na narudia leo kusisitiza kwamba msimamo bado ni ule ule. Hata baada ya korona watu bado wanakufa kwasababu hakuna anayejua kesho yake,” alisema na kuongeza.
“ Kama mwanafunzi yuko shule ya msingi atamaliza darasa la saba bila kulipa ada na kama yuko sekondari atamaliza kidato cha nne bila kulipa ada
Spread the love RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...
By Mwandishi WetuMarch 29, 2023Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...
By Mwandishi WetuMarch 29, 2023Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...
By Mwandishi WetuMarch 29, 2023Spread the love WAKATI serikali ikiweka mikakati mbalimbali kuimarisha sekta ya kilimo...
By Faki SosiMarch 28, 2023
Leave a comment