December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waliopata daraja la kwanza mitihani ya Taifa Ipepo Sekondari wakabidhiwa zawadi

Wanafunzi wa shule ya msingi

Spread the love

 

WADAU wa elimu kata ya Ipepo Wilaya Makete Mkoani Njombe wametimia ahadi ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wa Sekondari ya Ipepo waliopata ufaulu wa daraja la kwanza katika mitihani ya taifa ya kidato cha pili na cha nne mwaka 2021. Anaripoti Kenneth Ngesele, Makete … (endelea).

Zawadi hizo ni pamoja na kulipia ada  wanafunzi wawili waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano na kununua mahitaji ya shule kwa wanafunzi sita kidato cha tatu waliofanya vizuri kwa kupata daraja  la kwanza katika Mitihani ya taifa kidato cha pili.

Walio lipiwa ada na vifaa vya shule baada ya kuchaguliwa kujiunga kidato cha tano ni Osmeck  Edilo Sanga na Edsa  huku wanafunzi wa kidato cha tatu walipata daraja la kwanza na Mtihani wa taifa wa kidato cha pili ni Elia Jecko Sanga, Agano Yusuph Sanga, Ahadi Keidini Sanga na Victoria Ombeni Sanga.

Akizungumza kwa niaba ya wadau wa Maendeleo katika kata ya Ipepo Wilayani Makete, Mwalimu Alten Ntulo ambaye ni mwalimu wa Sekondari ya Njombe amesema kuwa wamekabidhi ada pamoja na vifaa kwa wanafunzi hao kwa lengo la kutimiza ahadi waliotoa mwaka jana.

Ntulo amesema kuwa walitoa ahadi hiyo mwaka jana siku walipotembelea shule hiyo kwa ajili ya kukabidhi vifaa vya maabara vyenye thamani ya Sh. 1.5 milioni kama zawadi baada ya shule hiyo kufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha pili mwaka jana kwa kushika nafasi Kiwilaya.

“Kiufupi tuliahidi kutoa zawadi kwa watakaopata daraja la kwanza  kidato cha nne katika mtihani wa taifa mwaka 2021 na wamechaguliwa kujiunga kidato cha tano,lakini tumetoa vifaa kama vile daftari counter book, lakini mdau Paulo Sanga alitoa pia vifaa kama vile, Begi za daftari kwa wanafunzi wa kidato cha pili waliopata daraja la kwanza’ amesema Ntulo.

Naye Paulo Sanga ambaye ni miongoni mwa wadau walioshiriki kununua vifaa hivyo amesema kuwa wao kama wadau hawataishia hapo bali wataendelea kutoa zawadi ya ada yote  na mahitaji mengine kwa wanafunzi watakaofanya vizuri na kuchaguliwa kuendelea na kidato cha tano.

“Lengo ni kuhamasisha ubora wa elimu nyumbani kwetu kata hasa kata ya Ipepo tulianza na kutoa vifaa vya mahabara mwaka  2021 na leo tumetoa kwa watoto nane waliofanya vizuri kwa kupata daraja la kwanza Wawili kidato cha nne na sita kitato chan pili,” amesema Sanga.

Kwa upande wake mratibu wa Elimu kata ya Ipepo Frotheus Mayemba amesema misaada ilitolewa na wadau  imekuwa chachu  na faraja kwa wanafunzi na walimu hususani shule ya sekondari Ipepo kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa kwa kidato cha pili na tatu.

Mayemba amesema mbali na zawadi kwa wanafunzi waliofanya vyema lakini pia wadau wengine Methew Msigwa ametoa msaada wa sola wati 120 na Paschal msingwa ametoa pikipiki kwaajili ya shule hiyo.

error: Content is protected !!