August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waliomuua Dk. Mvungi kuanza ‘kukaangwa’

Nyundo ya hakimu

Spread the love

UPELELEZI wa kesi ya mauaji ya kukusudia ya Dk. Sengondo Mvungi aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam umekamilika, anaadika Faki Sosi.

Mbele ya Thomas Simba Hakimu Mkazi Mkuu, Pamera Shinyambala ambaye ni wakili wa serikali, amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika hivyo ameiomba mahakama ipange tarehe kwa ajili ya kusikiliza maelezo ya mashahidi.

Miongoni mwa washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Chibago Magozi (32), John Mayunga (56), Juma Kangungu (29), Paulo Mdonondo (30), Mianda Mlewa (40), Zacharia Msese (33), Msungwa Matonya (30) na Ahmad Kitabu (30).

Katika orodha hiyo yumo pia Longishu Losingo aliyekuwa mlinzi wa Dk Mvungi, dereva na mkazi wa Kitunda, Masunga Makenza (40) ambapo kesi hiyo itaendelea tarehe tena tarehe 29 Desemba 2016.

Inadaiwa kuwa, kwa pamoja watu hao walimshambulia kwa mapanga na hatimaye kumsababishia kifo Dk. Mvungi mnamo tarehe 3 Novemba, mwaka 2013. Wanadaiwa kufanya kosa hilo la mauaji kinyume cha kifungu cha 196 cha Sheria na Kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

error: Content is protected !!