Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waliolipia 27,000 kabla ya mabadiliko ya bei kuunganishiwa umeme
Habari za Siasa

Waliolipia 27,000 kabla ya mabadiliko ya bei kuunganishiwa umeme

Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato
Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imesema imetoa maelekezo kwa mameneja wote wa mikoa na wilaya kuwaunganishia umeme wale wote waliokuwa wameshalipia Sh 27,000 kabla ya mabadiliko ya bei. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo Alhamisi tarehe 19 Mei 2022 na Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma.

Serikali ya awamu ya sita ilibadilisha bei ya kuunganisha umeme katika maeneo ya pembezoni mwa miji kutoka Sh 27,000 za awali na sasa itategemea na umbali wa kutoka kwenye nguzo. Hivi sasa bei hiyo imebakia kwa maeneop ambayo yapo katika vijiji kiutawala.

“Naomba niweke wazi hili kwamba wale wote waliokuwa wamelipia Sh 27,000 kabla ya mabadiliko ya bei waunganishiwe umeme kwa bei hiyo na maelekezo yameshatolewa kwa mameneja wa mikoa na wilaya,” amesema.

Amewataka kuzingatia kuunganisha wale walioanza kupeleka maombi na wateja ambao wamekaa muda mrefu bila kuunganishiwa wawasiliane na Serikali ili kuona tatizo lilipo.

1 Comment

  • Asante ndugu lakini uwelewe badhi inafika mwaka hatujaunganishiwa umeme na tumelipia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!