October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waliokula chakula cha sumu, afya zao zaimarika

Hospitali ya Rufaa ya Dodoma

Spread the love

WATU 53 wanaosadikiwa kula chakula chenye sumu katika msiba kata ya Mtumba Jijini Dodoma na kukimbizwa katika hospitali ya Rufaa, afya zao zimeimarika na wataruhusiwa wote leo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hali ya wagonjwa hao kuimarika imetolewa jana na mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa Jijini Dodoma, Dk Ibenzi Ernest alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya maendeleo ya wagonjwa hao.

Dk. Ibenzi alisema kuwa baada ya kuwapokea wagonjwa hao wanaosadikiwa kula chakula hicho na kuwa na mchafuko wa matumbo na kupatiwa matibabu kwa karibu, sasa wanaendelea vizuri. 

Hata hivyo Mganga huyo, alisema baada ya kupokea wagonjwa hao imeudwa timu ya wataalamu wa magonjwa ya tumbo kuona ni kitu gani kilichosababisha kuwapo kwa magonjwa hayo.

“Pamoja na kuundwa tume hiyo bado jamii inatakiwa kuwa makini katika maandalizi ya chakula kulingana na hali ya hewa ya mvua.

“Kwa matibabu ambayo wamepatiwa wagonjwa hao wote wana afya njema na tunategemea kuwaruhusu leo na inaonesha ni hali ya kawaida abayo inaweza kujitokeza kulingana na maadalizi yaliyofanyika,” alieleza Dk. Ibenzi.

Awali juzi watu 53 walilazwa  katika hospital ya Rufani ya Dodoma kwa kile kilichooelzwa kula chakula chenye sumu.

Watu hao no  wakazi wa eneo la Mtumba nje kidogo ya Jiji la Dodoma, wanadaiwa kukumbwa na mkasa huo ikiwa ni muda mfupi baada ya kula chakula katika msiba uliotokea eneo hilo.

Juzi Mganga Mkuu wa hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Best Magoma,  alithibitisha kupokea watu hao.

Dk. Magoma alisema hatua za awali zilizofanyika ni wagonjwa hao kupata tiba ya huduma ya kwanza huku taratibu za kupima sampuli ya chakula walichokula ukiendelea.

“Tutapima unga uliotumika kupika chakula pamoja na maharage na mboga za majani aina ya  ‘chanise’ chakula kinachodaiwa kutumiwa na wagonjwa hawa jana usiku.” Alifafanua Dk. Magoma.

Taarifa zaidi toka eneo la Mtumba zinadai watu hao walikula chakula katika msiba wa marehemu Edward Madumba, mkazi mwenzao kijijini hapo.

Dk. Magoma alisema, tayari wameunda timu ya ambayo imeenda kuchukua mabaki ya vyakula kwa ajili ya kupima ili kama ni sumu kuvu au ni ile ya kuwekwa na mtu.

“Tunashukuru hakuna kifo kilichotokea na chakula hiko walikula jana ucku na hivi sasa wote wanaendelea na drip za maji na dawa walizowekewa,”alisema Dk. Magoma.

Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Morroto alisema idadi ya wagonjwa imeongezeka na kufikia 53.

Alisema baada ya kutembelea wodini amebaini wagonjwa waliokutwa na dhahama hiyo ni 53 na kuongeza idadi hiyo inaweza kuongezeka.

Naye Meya wa jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe alisema anashukuru jitihada madaktari wa hospitali hiyo waliofanikiwa kuokoa maisha ya watu hao ambao wanahara na kutapika kutokana na kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi, alisema wanasubiri taarifa ya vipimo vya unga na maharagwe yaliyotumika kupikia kwenye msiba huo.

Hata hivyo amewashukuru madaktari wa General kutokana na jitihada za huduma ya kwanza iliotolewa kuhakikisha wagonjwa hao wote wamepata huduma.

error: Content is protected !!