Tuesday , 30 May 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Waliokufa kwa maporomoko Sierra Leone wazikwa
Kimataifa

Waliokufa kwa maporomoko Sierra Leone wazikwa

Kikosi cha uokoaji kikiendelea kuokoa majeruhi wa Maporomoko ya udongo huko Sierra Leone
Spread the love

NUSU ya maiti 400 zilizotokana na maporomoko ya udongo na mafuriko nje ya mji wa Freetown tayari zimezikwa, anaandika Hamisi Mguta.

Serikali nchini humo ilisema mazishi ya pamoja yangeahirishwa hadi leo ili kutoa fursa kwa ndugu na jamaa kutambua miili ya maiti ya waathirika.

Lakini mkuu wa wataalamu wa magonjwa kutoka mjini Freetown ameliambia shirika la habari la BBC kuwa baadhi ya mazishi yalikuwa yamekwishafanyika.

Imefahamika kuwa mazishi hayo yamehusisha miili ambayo tayari ilitambuliwa au ilikuwa imeharibika kabisa.

Watu wapatao 600 mpaka sasa hawajulikani walipo huku Rais wa Sierra Leone ametangaza siku saba za maombolezi.

Nathaniel Williams ni daktari katika hospitali kuu ya Connaught, iliyopo Freetown, anasema hivi sasa kuna tahadhari kubwa ya kutokea magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu hivyo sasa kunahitajika madawa na vyakula, kwa wale walioathirika.

Hata hivyo, Umoja wa Mataifa nchini humo umesema tayari umeweka mikakati ya kuweza kukabiliana na magonjwa ya milipuko iwapo yatatokea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Mkutano wa Quad Hiroshima waibuka na kutafuta amani na ustawi wa Indo-Pacific

Spread the love  JITIHADA za mazungumzo ya Pande Nne (Quad), hazikuthaminiwa na...

KimataifaTangulizi

Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda akamatwa Afrika Kusini

Spread the love  MMOJA wa watuhumiwa wakuu wa mauaji ya Kimbari ya...

Kimataifa

Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini China chaongezeka

Spread the love  WAKATI kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana nchini...

Kimataifa

Kampuni za kigeni zahofia kuendelea na biashara China

Spread the love OPERESHENI ya kiuchunguzi inayofanywa na Serikali ya China kwa...

error: Content is protected !!