JUMLA ya wanafunzi 12249 waliofaulu kuingia kidato cha kwanza na kukosa nafasi katika chaguo la kwanza mwaka huu kutokana na upungufu wa madarasa pamoja na madawati, watapata nafasi ya kujiunga baada ya madarasa na madawati kukamilika. Anaandika Eunice Laurian … (endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecksadik amesema walishindwa kuwapeleka wanafunzi hao shuleni kutoka na uhaba wa madarasa na madawati.
Amesema wanatarajia ifikapo mwisho wa wiki hii kuwa madarasa ambayo yalikuwa hayajakamilika yatakuwa yamekamilika na kamati husika itakaa tena na kupanga wanafunzi hao katika shule mbalimbali.
Ameonya kuwa kutokana na serikali kufuta ada na michango yote, wazazi hawatakuwa na kisingizio chochote cha kukosa tokuwapeleka watoto shule na kwa yeyote ambaye hatampeleka mtoto shule atakumbana na mkono wa sheria.
Aidha amewataka wazazi kuchangamkia fursa hiyo kwa kuwapeleka watoto wao shuleni pale tu watakapokuwa wamechaguliwa na kila moja atapelekwa pale atakapopangiwa na kamati husika.
More Stories
Wanafunzi walilia madarasa Mtwara, Silinde awajibu
Shule yenye darasa moja tangu 2014
Bweni lamuweka matatani Mkuu wa Shule Naliendele