December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waliofaulu darasa la saba 2021 wachaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2022

Wanafunzi wakishangilia baada ya kumaliza mtihani wa darasa la saba

Spread the love

 

JUMLA ya wanafunzi 907,802 waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu wamechaguliwa kujiunga na kidato cha mwaka mwaka 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akitangaza uchaguzi huo leo tarehe 24 Novemba, 2021, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Ummy Mwalimu amesema serikali itatoa kipaumbele kwa wanafunzi wa vijijini shule za kitaifa za bweni.

Amesema katika wanafunzi hao wamepangiwa kuanza masomo Januari 17, 2022 kwa wakati mmoja baada ya maandalizi ya Serikali.

Kati ya wanafunzi hao 907,802, wasichana ni 467,967 na wavulana 439,835 ambao ni sawa na asilimia 81.97 ya wanafunzi waliofanya Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka 2021.

“Kati ya waliofaulu na kupangiwa kujiunga na kidato cha kwanza wamo wanafunzi wenye mahitaji maalum 2,673 sawa na asilimia 0.29 ambao kati yao wavulana ni 1,471 na wasichana 1,202.

“Kwa mwaka 2022 kumekuwa na ongezeko la wanafunzi 73,932 sawa na asilimia 8.87 ya wanafunzi waliofaulu ukilinganisha na mwaka, 2020 ambapo jumla ya wanafunzi 833,872 walifaulu na kupata sifa ya kujiunga na masomo ya Kidato cha Kwanza,” amesema.

WaziriI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu

Aidha, amesema upangaji huo utahusisha wanafunzi wenye ufaulu mzuri zaidi ambao wao watapangiwa kulingana na alama zao na kwa mwaka 2022 wanafunzi waliofaulu zaidi na kupangiwa ni wanafunzi 4188.

“Wanafunzi waliopangiwa shule za bweni za Kitaifa ni 1989 na hapa tumechukua zaidi wanafunzi wa vijijini lakini kwenye majiji na halmashauri tumeangalia sana wenye uhitaji tu,” amesema.

Amesema sababu za kupangiwa zaidi kwa wanafunzi wa vijijini katika shule za bweni za Kitaifa kwamba kunatokana na uamuzi wa Serikali wa kujali wanafunzi wote wapate elimu.

  • Kupata majina ya wanafunzi na shule walizochaguliwa ingia hapa

“Mpango wa kupanga nafasi hizo unakwenda kusaidia wanafunzi ambao huwa kwenye mazingira magumu na vikwazo ili wasome,” amesema.

Pia ameagiza wakuu wa shule kote nchi kuacha visingizio vya michango au sare kwa wanafunzi wanaoanza bali waachwe waendelee na masomo huku mambo mengine watakamilisha mbeleni.

error: Content is protected !!