December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waliochoma Kituo cha Polisi  Bunju A wafungwa maisha

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Februari 2019 imewafunga maisha jela watu wanane baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya kuchoma moto Kituo cha Polisi cha Bunju A kilichopo jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hukumu hiyo iliyoacha simanzi imetolewa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Simba amesema kitendo cha watu hao kuchoma kituo hicho hakivumiliki na kushindwa kuwaonea huruma kutokana na kuhatarisha usalama wa nchi.

Washtakiwa hao walitekeleza tukio hilo tarehe 10 Julai mwaka 2010, ambapo walikuwa wanakabiliwa na mashtaka sita ikiwemo shtaka hilo la kuchoma moto kituo hicho.

Mbali na washtakiwa hao nane kufungwa maisha jela, Mahakama imewaacha huru watu 10  walioshtakiwa kwa kosa hilo. Awali wakati kesi hiyo inafunguliwa, kulikuwa na washtakiwa 35 ambapo 17 waliachwa huru na kubaki 18, ambapo leo hii kumi waliachwa huru pia baada ya kuonekana hawana hatia.

error: Content is protected !!