January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Walinzi wa Rais Mugabe wasimamishwa kazi

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe akianguka jukwaani

Spread the love

KUANGUKA kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kumepelekea maafisa usalama 27 kusimamishwa kazi wakatii uchunguzi ukiendelea. Maafisa hao wamekabidhiwa barua za kusimamishwa  siku ya Ijumaa.

Mmoja wa maafisa alisema kuwa baadhi ya watu wanalichukulia tukio hili kirahisi lakini hili ni swala zito na linapaswa kushughulikiwa. “Ninawasiwasi kama watarudi kazini, maafisa usalama walijisahau, walichukulia mambo kirahisi na wakashindwa kuzingatia misingi ya usalama.

“Ni protokali kwa mlinzi binafsi wa Rais kuwa umbali usiozidi mita 3 kwani wapambe hawa ni muhimu kumkinga Rais kwa risasi kwa kutumia miili yao kama kinga, pia wanajukumu la kuzuia Rais asianguke kwa kutumia mikono yao au mabega”.

“Alianguka kwa kushika ardhi, hii haikubaliki” ofisa huyo alisikika. Maafisa hawa wameshindwa kuzingatia Kanuni namba 3, inayopatikana kwenye makabrasha yao ya mafunzo, kanuni hiyo inaeleza umbali wanaotakiwa kusimama wakiwa na Rais.

Mugabe alianguka uwanja wa ndege wa Harare akitokea Ethiopia alipoenda kuchukua nafasi ya uenyekiti wa Umoja wa Nchi za Afrika. Mugabe alianguka wakati anashuka kwenye ngazi baada ya kuwahutubia washabiki na wanachama wa Zanu PF waliokuja kumpongeza.

error: Content is protected !!