MALI imeendelea kuwa na usalama hafifu hali iliyolazimu Ujumbe wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa (MINUSMA) nchini humo, kuondoka leo Jumatatu kutokana na mashambulizi yanayohatarisha ulinzi wao. Anaripoti Mlelwa Kiwale, TUDARCo, kwa msaada wa Mitandao ya Kimataifa…(endelea).
Hatua hiyo imejiri baada ya jeshi la Mali (FaMa) kusema takribani wanajeshi wao wanane wamejeruhiwa na wengine saba wameuawa katika mashambulizi yaliyoyafanywa na waasi wa zamani kupitia uongozi wa kikundi cha waasi cha Azawad (CMA).
Pia wanajeshi wa nchi hiyo waliwaua waasi takribani 28 na kuweka ulinzi katika mji wa Ber ambapo uliokaliwa na kikosi hicho cha kulinda amani nchini humo.
Kikosi hicho kilisema msafara wao ulishambuliwa mara mbili na watu wao watatu kujeruhiwa na kupelekwa hospitalini Timbuktu kwa matibabu zaidi.
Hivyo, mashambulizi hayo yaliwawalazimu wao kuondoka mapema katika mji wa Ber kaskazini mwa mali.
Leave a comment