January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Walimu watangaza kuinyima kura CCM

Spread the love

CHAMA cha Walimu Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, kimesema kitendo cha serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuwapiga `chenga` kila kukicha, watahakikisha wanawashinikiza walimu na wanafunzi wa sekondari, kuacha kukipigia kura Oktoba 25, 2015. Anaandika Moses Mseti, Magu … (endelea).

Malalamiko ya walimu hao yanakuja ikiwa ni wiki mbili sasa tangu kutolewa tamko na uongozi wa chama hicho Taifa kuitaka serikali kulipa deni la Sh. 19 billioni ambalo ni la nchi nzima lakini siku chache serikali ilikanusha kudaiwa fedha hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa CWT, Magu, Coroneli Magembe amesema wamevumilia vya kutosha na sasa wamechoka na ahadi za serikali zisizotekelezeka kila kukicha hivyo kuanzia Oktoba watagoma na kushinikiza walimu kuacha kuichagua CCM.

Amesema walimu wilayani magu wanaidai serikali zaidi ya Sh. 500 milioni ambazo ni za malimbikizo ya mishahara, fedha za likizo, kujikimu, uhamisho na fedha za walimu kwenda masomoni.

Magembe amesema wamekuwa wakizungumza na Mkurugenzi wa wilaya, Paulo Ntinika lakini amekuwa akiwapiga kalenda na kuwapa majibu yasiyoridhisha kitendo ambacho kinawakatisha tamaa walimu hao na kulazimika kuanza mgomo na kuchukua maamuzi ya kushinikiza walimu wasikipigie kura.

Hata hivyo Magembe amesema wamemuandikia mkurugenzi barua ya kuanza mgomo kuanzia Oktoba mosi na kuendelea mpaka pale watakapopata stahiki zao, pia hata kama wakilipwa hawata kipigia kura chama tawala.

Amesema hata kama watalipwa stahiki zao watamburuza mkurugenzi huyo katika vyombo vya dora kutokana na kushindwa kuteleza wajibu wake wa kusimamia kazi za umma na badala yake amekuwa ni kiongozi anayetumikia kabila moja (limehifadhiwa kwa ajili ya usalama).

“Tumemwandikia barua ambayo tumetoa mwezi mmoja, huu wa Septemba na kuanzia Oktoba mosi sisi walimu wote tutashinikiza wagome, kama wanaona ni raha walimu kuishi maisha bila stahiki zao, waingie darasani wafundishe na wao,” amesema Magembe.

Mwenyekiti wa CWT Magu, Christopher Mwakitonga, yeye alimtuhumu kwa madai mengine Mkurugenzi huyo kwamba ameshindwa kurejesha fedha za makato ya mishahara ya walimu ambayo yalikuwa yanakatwa na kuwekwa katika mfuko wa Inuka Mwanamke.

Amesema Mfuko wa Inuka Mwanamke ulianzishwa Mwaka 2001 kwa lengo la walimu wanawake kujikwamua kiuchumi cha kushangaza fedha zilizokuwa zikikatwa kwenye mishahara yao na kuingia katika mfuko huo tangu 2014 mpaka sasa hazionekani.

Mwakitonga amesema makato waliyokuwa wakikatwa walimu hao ni Sh. 5000 lakini hali ilibadilika wengine wakaanza kukatwa 10,000, lakini walipokwenda kuuliza sehemu husika majibu yaliyokuwa yakitolewa sio ya kuridhisha.

error: Content is protected !!