August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Walimu wataka DED aliyempigisha deki mwenzao ang’oke

Gratian Mukoba, Rais wa Chama cha Walimu Tanzania

Spread the love

KITENDO cha Eliud Mwaiteleke, Mkurugenzi wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kumpigisha deki mwalimu, kimeibua maandamano, anaandika Moses Mseti.

Chama cha Walimu (CWT) wilaya humo kimetangaza maandamano kushinikiza Mwaiteleke aondolewe katika nafasi yake.

Tarehe 17 Oktoba mwaka huu Mwaiteleke alimpigisha deki Mwalimu Hamis Sengo wa Shule ya Sekondari ya Shilala mbele ya wanafunzi na watendaji wa halmashauri hiyo.

Mwaiteleke aliyekuwa ameambatana na maofisa wa serikali wa wilaya hiyo, alifika shule hapo jioni, muda ambao wanafunzi wa Kidato cha Nne walikuwa darasani wakijisomea.

Baada ya mkurugenzi huyo kufika shuleni hapo, alikuta madarasa yakiwa machafu na kumuita mwalimu (Sengo) kueleza sababu za madarasa hayo kuwa machafu na ndipo alipomtaka kudeki kitendo kilichotekelezwa na Sengo.

Tukio lingine lilitokea tarehe 21 na 22 Oktoba mwaka huu ambapo mkurugenzi aliwapigisha deki chooni walimu watano wa Shule ya Msingi ya Ntulya kwa madai kwamba, baadhi ya vyoo hivyo alivikuta vichafu.

Akizungumza na mtandao huu leo Sibora Kisheria, Mwenyekiti wa CWT mkoani Mwanza amesema kuwa, wanafanya maandamano ili kushinikiza mkurugenzi huyo kufukuzwa kazi kutokana na vitendo vyake vya unyanyasaji.

“Huu sio utendaji kazi bali ni unyanyasaji mbaya unaofanywa na mkurugenzi (Mwaiteleke), hatutakubali kuona vitendo hivi vikiendelea kufanyika kwa walimu wetu sehemu yeyote ile,” amesema Kisheri na kuongeza;

Amesema kuwa, wameamua kufanya maandamano hayo ili kuhakikisha walimu mkoani humo na nchini kwa ujumla hawanyanyaswi na kudhalilishwa na viongozi walio juu yao.

Sengo amesema kuwa, katika kikao cha viongozi wa CWT wa ngazi za wilaya na mikoa kilichofanyika mkoani Dodoma, waliadhimia mambo kadhaa.

Baadhi ya mambo walioadhimia ni mkurugenzi huyo amhamishe mwalimu aliyenyanyaswa kwa gharama zake na kutofanya vitendo hivyo kwa walimu wengine katika wilaya hiyo na sehemu yoyote.

error: Content is protected !!