July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Walimu wapigiwa chapuo bungeni

Mwalimu akiwa darasani

Spread the love

IMEPENDEKEZWA Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), iruhusiwe kulipa mishahara ya walimu badala ya Serikali. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Mapendekezo hayo yalitolewa leo bungeni na baadhi ya wabunge ambao walikuwa wakijadili muda mfupi baada ya kuwasilishwa bungeni kwa Muswada wa Kutunga Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu wa Mwaka 2015.

Wabunge hao wamesema iwapo TSC itapewa jukumu hilo, itakuwa ni njia pekee ya kuifanya tume hiyo itimize majukumu yake ipasavyo kutokana na sheria kuwaruhusu kuajiri na kusimamia walimu wote nchini

Mapendekezo hayo yalitolewa na wabunge hao walipokuwa wakichangia Muswada wa Kutunga Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu wa Mwaka 2015.

Akichangia mbunge wa Viti Maalum Magreth Mkanga (CCM) alisema majukumu ya TSC yatakamilika iwapo itaruhusiwa kulipa mishahara ya walimu.

Amesema kwa kuwa muswada umeeleza bayana kuwa majukumu ya tume yatakuwa ni pamoja na kuajiri, kupandisha vyeo na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya walimu, ni vyema sasa tume iruhusiwe kulipa mishahara ya walimu .

“Nasema hivyo kwa sababu huwezi kumpa mtu jukumu la kuajiri na kusimamia, halafu ukamnyima haki ya kulipa mshahara, hilo haliwezekani,” amesema Mkanga.

Wabunge hao wakichangia ambapo Mbunge wa Viti Maalum, Zainab Kawawa (CCM) na Mbunge wa Igunga, Dk. Hamis Kigwangala ambao walitoa sababu zinazofanana na zilizotolewa na Mkanga.

Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Magreth Sitta, alipokuwa akiwasilisha maoni ya kamati yake juu ya muswada huo, naye aliitaka Serikali iiruhusu TSC ilipe mishahara ya walimu pamoja na kuwasambaza mikoani kulingana na mahitaji.

Nae Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM), aliitaka Serikali iwe na utaratibu wa kuajiri walimu wenye ufauru wa daraja la kwanza badala ya utaratibu wa sasa unaoruhusu wahitimu waliofauru kwa madaraja ya chini kuajiriwa katika ualimu.

error: Content is protected !!