August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Walimu wanaorubuni wanafunzi kukiona

Mwanafunzi mwenye Mimba

Spread the love

SERIKALI Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma  imeahidi kuwachukulia hatua za kisheria walimu wote ambao watatajwa kujihusisha kimapenzi na watoto wa kike wanaosoma katika shule zote, anaandika Mwandishi Wetu.

Aidha, amewataka walimu ambao wanajiona kuwa na mahitaji ya kufanya mapenzi na hawajui maeneo ya kupata wanawake kupeleka maombi ofisini kwake na yeye atafanya taratibu za kuwatafutia wanawake ambao wamekuwa wakijiuza.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Juma Homera wakati akizungumza na wanafunzi na walimu wa shule ya Sekondari Mtutura iliyopo katika Kata ya Namiungo wakati alipofanya ziara ya ukaguzi na uhamasishaji wa maendeleo.

Katika taarifa hiyo Dc, Homera aliitaja Shule ya Kutwa ya Frank Weston mini hapa kuwa imekuwa ni miongoni mwa shule zinazotajwa kuwa ni kituo cha Mapenzi kati yao na wanafunzi.

Amesema walimu wanne wa shule hiyo ingawa hakuwataja majina yao wamekwisha simamisha kazi baada ya kutuhumiwa kuwa na mahusiano na wanafunzi shuleni hapo.

Hata hivyo, Homera aliwataka watoto wa kike kuzingatia masomo na kwamba endapo watashindwa kusoma wajue kwamba wameumia kwani watashindwa kuzifikia ndoto zao kielimu.

Amesema ndoto zao hazitazimia endapo watabainika kupata ujauzito kwa kuwa serikali ina mpango wa kuwapima kipimo watoto wote wa kike wiki mbili au moja kabla ya kipindi cha kufanya mitihani ya kidato cha Pili na cha Nne kila mwaka na kuwaondoa watakaobainika kuwa na mimba.

error: Content is protected !!