Tuesday , 27 February 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Walimu walionyimwa stahiki zao wamchongea Mkurugenzi kwa Jafo
Elimu

Walimu walionyimwa stahiki zao wamchongea Mkurugenzi kwa Jafo

Suleiman Jafo, Waziri wa Tamisemi
Spread the love

WALIMU watano waliohamishwa kutoka kituo cha kazi cha shule ya sekondari Kisasa katika Jiji la Dodoma na kupangwa kwenye vituo vingine bila kulipwa stahiki zao za uhamisho, wamepeleka kilio chao kwa Waziri wa TAMISEMI, Suleiman Jafo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kutokana na hali hiyo walimu hao (wameomba majina yao yahifadhiwe) wamemuomba Waziri Jafo kuingilia kati jambo hilo kwani inaonekana kuna dalili za kutaka kufukuzwa kazi kwa mizengwe.

Hali hiyo imejidhiilisha baada ya walimu wa shule ya sekondari Kisasa Jijini Dodoma kuhamishwa na kupelekwa katika vituo vingine vya kazi bila kulipwa stahiki zao za uhamisho kama ilivyoelekezwa na Rais Magufuli.

Walimu hao walikuwa ni walimu wa shule hiyo na kuhamishwa kwa siku moja bila kulipwa stahiki zao za uhamisho, kama ilivyoagizwa na Rais Magufuli, alilolitoa Mei Mosi 2017 katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi wilaya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Maagizo hayo ya Rais ya kutaka watumishi kutohamishwa bila kulipwa stahiki zao iliwekewa mkazo na Waziri wa Jafo, wakati akijibu maswali ya wabunge bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu alipokuwa akijibu maswali ni kwanini walimu na baadhi ya watumishi wamekuwa wakihamishwa bila kupewa stahiki zao za uhamisho.

Wakizungumza na MwanaHALISI Online walimu hao, walisema kuwa kitendo cha kuhamishwa bila kupewa fedha ni kwenda kinyume na utaratibu wa kazi.

Kwa Mujibu wa  walimu hao walipata walisema kuwa kwa pamoja walipata barua za uhamisho Julai 17 mwaka huu zenye maelezo kuwa uhamisho wao utagharamiwa na serikali jambo ambalo halijafanyika.

“Sisi walimu hatujakataa kuhama lakini hatujalipwa fedha zetu lakini hatuna fedha za kujikimu na vituo vipo mbali na hatuna hata fedha za kulipa kodi,” walisema walimu hao.

Wakiendelea kuelezea walimu hao walisema licha ya kutokulipwa stahiki zao za uhamisho walidai kuwa wamefikia hatua ya wakuu wa shule katika vituo vipya wamekuwa wakizuiliwa kusahini katika daftari ya Maudhurio.

Alipofafutwa Afisa Elimu Sekondari Jiji la Dodoma, Martin Nkwabi ili aweze kuelezea ni kwanini walimu hao wamehamishwa watano kwa wakati mmoja kutoka shule moja na kutokulipwa stahiki zao za uhamisho alijibu kuwa aulizwe Mkurugenzi wa Jiji ambaye ni Godwini Kunambi na kukata simu.

Alipotafutwa Mkurugenzi wa Jiji Godwini Kunambi, hakupokea siku na alipotumiwa ujumbe mfupi kwa simu ya kiganjani hakuweza kujibu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Walimu (CWT) Mkoa wa Dodoma, Samson Mkotya, alisema kuwa hana imani kuwa kuna mtumishi ambaye anaweza kukaidi kutekeleza agizo lililotolewa na Rais Dk. John Magufuli na kuungwa mkono na Waziri wa TAMISEMI pamoja na kutolewa Maagizo na Waziri wa Utumishi na Utawala Bora.

“Napenda kusema kuwa walimu kuhamishwa kwa wakati mmoja siyo tatizo hiyo inatokana na mahitaji lakini kinachotakiwa ni kuwa na utaratibu ambao unatakiwa wa kuwahamisha walimu hao.

“Sipendi kuhamini kuwa ofisi ya Ofisa Elimu na ofisi ya Mkurugenzi ambao tumekuwa tukifanya nao kazi vizuri kwa kushirikiana wanawahamisha walimu hao bila kufuata utaratibu wa kisheria uliowekwa,” alieleza Mkotya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Takukuru wambana Mwalimu mkuu, atema bungo

Spread the loveMwalimu Mkuu wa shule msingi Hanihani, kata ya Igunga wilayani...

ElimuHabari za Siasa

Prof Muhongo ataka ubunifu mitaala mipya ya elimu

Spread the loveSERIKALI imetakiwa kuhakikisha  maarifa, ujuzi, uvumbuzi na udadisi vinazingatiwa kwenye...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa saidizi kwa walimu, wanafunzi wenye ulemavu Ilala

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi msaada wa vifaa saidizi kwa walimu...

Elimu

St. Mary’s Mbezi Beach High School yafanya maajabu kidato cha nne

Spread the love  WANAFUNZI waliomaliza  kidato cha nne kwenye shule ya sekondari...

error: Content is protected !!