Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Walimu walalama kufanya kazi wikiendi
Elimu

Walimu walalama kufanya kazi wikiendi

Spread the love

CHAMA cha walimu Wilayani Chamwino mkoani Dodoma (CWT), kimelalamikia walimu kufanyishwa kazi siku za mwisho wa wiki (wikiendi) bila malipo wala chakula kinyume na kanuni na miongozo ya kazi kwa mujibu wa sheria ya ajira na mahusiano kazini. Anaripoti Danson Kaijage, Chamwino … (endelea).

Malalamiko hayo yalitolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa CWT wilaya hiyo Clement Mahemba, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wilayani hapo

Mahemba alisema utaratibu huo ambao umeandaliwa na ofisa elimu msingi wa wilaya hiyo, umekuwa ukinyanyasa walimu kutokana na kuwatumikisha siku za mapumziko ambazo ni Jumamosi na Jumapili.

Alisema pamoja na walimu hao kutumikishwa kazi katika siku za kwenda kufanya ibada lakini pia katika mpango huo ambao afisa elimu huyo anauita kuwa ni vikao kazi, kumekuwa hakuna malipo yoyote wala chakula.

“Walimu wanafanyishwa kazi siku za Jumamosi pamoja na Jumapili siku ambazo wengi wao wanatakiwa kufanya mapumziko kwa ajili ya kujiaanda Jumatatu kwenda kufundisha,” alisema na kuongeza kuwa:

“Lakini pia walimu hawa wanatoka umbali mrefu kuna walimu wanatoka kijiji cha Champumba kwenda Mlowa barabarani ni zaidi ya kilomita 80 kwenda kushiriki hivyo vikao kazi hivyo kukosa muda wa kufanya maandalizi ya Jumatatu.”

Mahemba aliongeza kuwa kitendo cha mwajili kumwita mtumishi wake kazini siku za wikiendi anatakiwa kumlipa kama ambavyo sheria ya ajira na mahusiano kazini namba 6 ya mwaka 2004 kifungu cha 24(1)6 na 24(4) vinavyo elekeza.

“Ni lazima mwajili azielewe hizi sheria na kwanini wawanyime walimu hata kwenda kufanya ibada au kwa sababu mkurugenzi ni mwislamu pamoja na afisa elimu wake,” alihoji mwenyekiti huyo.

Akijibu malalamiko hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino, Athumani Massasi alisema kuwa anachofahamu yeye ni kuwa hakuna mwalimu aliyelazimishwa wote wanafanya hivyo kwa utayari wao.

“Ninacho kifahamu mimi mwandishi hawa walimu ni makubalianao yao hivyo hakuna mwalimu yeyote ambaye amelazimishwa kufanya hivyo wanavyofanya sasa lakini kama unataka kufahamu zaidi njoo ofisini,” alisema Massasi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

error: Content is protected !!