January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Walimu waitwa kununua hisa

Baadhi ya Walimu ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha walimu Tanzania Wilaya ya Njombe

Spread the love

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), kimeendelea kuwahamasisha walimu nchini kujitokeza kwa wingi kununua hisa katika benki yao tarajiwa, itakayojulikana kama Mwalimu Commercial Bank (MCB). Anaandika Mwandishi wetu, Dodoma  (endelea).

Akizungumza na walimu wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Meneja mradi, Ronald Manongi, amesema kuna haja kubwa ya walimu kujiunga na benki hiyo ili kuondokana na kadhia ya kukopeshwa kwa riba kubwa.

Manongi amesema benki hiyo imejipanga kwa ajili ya kumjali mwalimu na kumkomboa kutoka katika mikopo ya riba kubwa na kuingia katika mikopo nafuu.

Amesema, “licha ya mwalimu kuwa na mikopo nafuu, bado kutakuwepo na fursa ya kuwa mwanachama kutokana na hisa zake.

Naye mshauri mradi, George Fumbuka, amesema iwapo walimu watajitokeza kwa wingi kununua hisa katika benki hiyo, ni wazi watakuwa na uhakika wa kupata huduma ya kifedha yenye nafuu kuliko benki zote nchini.

Kwa mujibu wa Fumbuka, mpaka sasa zaidi ya walimu 217,771 wamenunua hisa ambapo kila mmoja amenunua zaidi ya 10.

Hata hivyo, baadhi ya walimu wameonesha wasiwasi kuwa kuna ujanja ambao unafanywa na baadhi ya viongozi wa Chama cha Walimu (CWT) kwa lengo la kujinufaisha.

Wakichangia hoja katika semina hiyo, walisema hakuna sababu ya kuwa na benki ambayo walimu hawakushirikishwa mchakato mzima wa kuanzishwa kwake.

error: Content is protected !!