Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Walimu waipongeza Serikali kulipa malimbikizo ya bilioni 117 , yataka kasi iongezeke
ElimuHabari

Walimu waipongeza Serikali kulipa malimbikizo ya bilioni 117 , yataka kasi iongezeke

Spread the love

 

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), kimeipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kulipa malimbikizo ya madai ya walimu 88,297 yenye thamani ya zaidi ya Sh. 117 bilioni, katika kipindi cha mitatu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Pongezi hizo zimetolewa leo Alhamisi, tarehe 15 Desemba 2022 na Kaimu Katibu Mkuu wa CWT, Mwalimu Japhet Manganga, akisoma risala ya walimu katika mkutano mkuu wa chama hicho, uliofanyika jijini Dodoma.

Mwalimu Maganga amesema, katika mwaka wa fedha wa 2020/21, jumla ya madai 30,825 yenye thamani Sh. 42.7 bilioni yalilipwa, wakati madai 53,383 yenye thamani ya zaidi ya Sh. 68 bilioni yalilipwa 2021/22, huku madai 5,089 yenye thamani ya Sh. 6.9 bilioni yalilipwa 2022/23.

Licha ya pongezi hizo, Mwalimu Maganga ameiomba Serikali kuongeza kasi ya malipo ya malimbikizo ya madeni yaliyosalia “tunaiomba Serikali kuongeza kasi ya kulipa madeni ya mishahara yaliyolimbikizwa kipindi cha nyuma, ili kuendana na mfumo wa sasa kwani athari za kutofanya hivyo ni kubwa.”

“Hasa kwa walimu ambao wamefikia umri wa kustaafu na wengine waliostaafu kabla ya kulipwa madeni, hivyo kuwawia vigumu kuendelea kuidai Serikali wakiwa nje ya mfumo wa utumishi,” amesema Mwalimu Maganga.

Aidha, Mwalimu Maganga, amesema walimu wanaipongeza Serikali kwa kufuta ada ya uhifadhi iliyokuwa inatozwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa wanufaika, kuongeza umri wa utegemezi wanaonufaika na mfuko wa bima ya afya ya taifa kutoka miaka 18 hadi 21 na kulipa michango ya wafanyakazi walioondolewa kazini kutokana na vyeti vya kughushi.

Pia, Mwalimu Maganga amesema walimu wanaipongeza Serikali kwa kupandisha pamoja na kuwabadilishia madaraja walimu, ambapo kwa 2020/21 walimu 117,847 walipandishwa vyeo na 2021/22 walipandishwa vyeo 42,300. Pia, walimu 14,172 walibadilishiwa kada 2020/21.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

RC Songwe ang’aka kesi 2 kati ya 60 za mafataki kuamuliwa

Spread the loveMkuu wa mkoa wa Songwe Dk. Fransis Michael ameshangazwa na...

error: Content is protected !!