January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Walimu wageuza shule ya umma mradi binafsi

Wakati walimu wa Kigogo Fresh wakikusanya fedha kwa wanafunzi, kuna baadhi ya shule za msingi za Tanzania hali yake ni hii

Spread the love

WALIMU katika Shule ya Msingi Kigogo Fresh iliyopo kata ya Pugu, Manispaa ya Ilala, nje ya jiji la Dar es salaam, wamelalamikiwa kugeuza mpango wa serikali wa kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi kuwa “mradi binafsi.” Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mtandao huu, wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wamesema, “pamoja na serikali kutangaza kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi, walimu wa shule hii wanawalazimisha wanafunzi kulipia gharama za masomo wanayoyaita ‘masomo ya ziada’” (tuition).

Abdiel Athumani, mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake anasoma katika shule hiyo anasema, wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu wanalipa Sh. 300 kwa siku. Darasa la tano na la sita wanalipa Sh. 800 na darasa la nne na la saba wanalipa Sh 1,000.

Mbali na gharama hizo, wazazi wenye wanafunzi wa darasa la saba wanalazimika kulipia sh 1,000 kila Jumamosi kama gharama za mitihani ya majaribio; uji kwa wanafunzi Sh. 200 na malipo kwa ajili ya mlinzi ni Sh. 200 kwa mwezi.

“ Mimi ni mlezi wa wanafunzi watatu. Wawili wapo darasa la saba na mmoja yupo darasa la pili. Nalazimika kulipia Sh. 54,600 kwa mwezi. Kazi yangu ni mlinzi. Mshahara wangu kwa mwezi ni Sh. 80,000. Wakati mwingine nashidwa kulipa hizi gharama. Watoto wangu wanaambulia viboko na adhabu za kung’oa visiki,” ameeleza mzazi mwingine kwa sharti jina.

Amesema, “Nalipia jengo, nalipia dawati. Nalipa hela ya mlinzi. Lakini walimu wanaendesha mradi wao kwenye majengo yetu. Kwa nini wasitafute majengo yao?”

Amesema gharama hizo ni mzigo mkubwa kwa wazazi wenye kipato cha chini. Anasema hali hiyo, inachangia utoro na kushuka kiwango cha elimu kwa wanafunzi hao.

Alipotafutwa mwalimu mkuu wa shule hiyo, Lilian Mmbando kwa njia ya simu na kutaka kujua ukweli kuhusu tuhuma hizo, alijibu kwa ufupi“…ni kweli gharama za masomo ya ziada zipo. Lakini sio hizo walizokueleza.”

error: Content is protected !!